Prof Issa Shivji aliyekuwa Mwenyekiti wa taasisi ya Kavazi la Mwalimu Nyerere amesema taasisi hiyo imefungwa rasmi baada ya kukamilisha majukumu yaliyosababisha ianzishwe.
Shivji amesema sasa fikra za mwalimu Nyerere zitaendelea kusomwa kupitia vitabu mbalimbali vilivyotayarishwa na taasisi hiyo badala ya semina na makongamano kama ilivyokuwa wakati wa uhai wa taasisi hiyo.
Source: ITV