HARUNI IDDI
Member
- May 31, 2024
- 8
- 3
Taasisi ya kuzuia na kumbana na rushwa (TAKUKURU) inapaswa kushirikia na wizara ya ujenzi kupitia wakala wa barabara (Tanroads) ili kudhibiti vitendo vya rushwa kati ya madereva na mafisa wa vituo vya kupima uzito wa magari ili kusudi miundombinu ya barabara hasa za mikoani kuweza kudumu kwa muda mrefu na kupunguza gharama za matengenezo yasiokuwa ya lazima kutoka na kuharibika kwa barabara Kama vile barabara kutoka mashimo, kukatika, na mda mwengine kutoka nyufa.
ZIFUATAZO NI FAIDA AMBAZO ZITATOKANA NA KUPAMBANA NA RUSHWA KATIKA VITUO VYA KUPIMA UZITO MAGARI
1. Kupunguza ajali ambazo husababishwa na ubovu wa barabara.
Ajali nyingi zimekuwa zikitokana na ubovu wa miundombinu ya barabara hasa kuwepo kwa mashimo, na uchakavu wa barabara hasa barabara za mikoani kutokana na uharibifu unaletwa na uzito uliopitiliza wa magari ya mizigo.
2. Kupunguza gharama za matengenezo yasiokuwa ya lazima ya barabara.
Serekali hutumia fedha nyingi kufanya ukarabati wa barabara zinazo haribika kutokana uzito wa magari kuharibu miundombinu na kutokana na ukosefu wa fedha kwenye mfuko wa barabara yaani (Road fund) kunapelekea uharibifu huo kudumu kwa mda mrefu na kuleta adha kwa watumiaji wengine wa barabara.
3. Kuongeza muda wa barabara kuishi ( increase road life span).
Ili miundombinu ya barabara iweze kudumu kwa muda mrefu ni muhimu kwa maafisa waliopo kwenye vituo vya kupima uzito wa magari (Mizani) kuwa wadilifu na TAKUKURU kuweka udhibiti wakusha ili kuweza kuzuia magari ambayo yanaweza kuharibu barabara yazuiwe kikamilifu ili kulinda maisha ya miundombinu ya barabara.
ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO ZINAWEZA KUDHIBITI VITENDO VYA RUSHWA KWENYE VITUO VYA KUPIMA UZITO WA MAGARI
1. Ufungaji wa kamera
Ili kudhibiti vitendo vya rushwa ambavyo hupelekea uharibifu wa miundombinu mbinu ya barabara ni muhimu kwa wakala wa barabara kuishirikana na jeshi la polisi kufunga kamera za usalama kwenye vituo vya kupima uzito magari ili kudhibiti vitendo vya rushwa ambavyo hupelekea uharibifu wa miundombinu ya barabara.
2. Kufutiwa leseni kwa madereva ambao watakuwa wanazidisha uzito kwa makusudi.
Ili kuweza kutokomeza swala hili ambalo limekuwa liki ongeza gharama za matengenezo na ukarabati wa barabara ni muhimu kudhibiti tabia ya madereva ambao wamekuwa wakaidi katika kubeba mizigo bila kufata sheria, kanuni na miongozo ya usafirishaji.
3. Kuwa chukulia hatua za kisheria watumishi wa Mizani.
Ili kupunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara Kuna haja yakuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi ambao watakuwa wanaenda kinyume na taratibu hasa kujihushisha na maswala ya rushwa.
ushirikiano kati ya TAKUKURU Tanroads kudhibiti vitendo vya rushwa katika vituo vya kupima uzito magari kunaweza kulinda miundombinu ya barabara kwa miaka 5 na kuendelea mbele.

Upvote
1