Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yaanza mchakato wa upandikizaji wa moyo nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeanza rasmi maandalizi ya kuanzisha huduma ya upandikizaji wa moyo, hatua hiyo imeelezwa kuwa inatarajiwa kuendelea kuiweka Tanzania kwenye ramani ya huduma za juu za moyo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza Julai 30, 2025 kuelekea maadhimisho ya Miaka 10 ya JKCI, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dkt. Peter *******, alisema kuwa mchakato huo ni wa kihistoria na utafungua ukurasa mpya katika utoaji wa huduma za matibabu ya moyo nchini.
WhatsApp Image 2025-07-31 at 14.56.31_bbf92d06.jpg
"Tayari tumezindua Kamati Maalum ya Upandikizaji wa Moyo itakayosimamia maandalizi yote ya kitaalamu, kisheria na kiutendaji ndani ya kipindi cha miaka mitano. Hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu na pia kwa nchi jirani ambazo hazina huduma hii," alisema Dkt. *******.

Aidha alifafanua kuwa huduma hiyo ya upandikizaji wa moyo inahitaji mchakato kwa kuwa yanatakiwa maandalizi makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji wa vifaa tiba vya kisasa, mafunzo ya wataalamu, pamoja na utaratibu wa kisheria na kimaadili.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Upandikizaji wa Moyo, Dkt. Evarist Nyawawa, alieleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utafuata mifumo bora ya kimataifa na kwamba tayari kuna takwimu zinaonesha kuwa watu zaidi ya 50,000 duniani wamekwishafanyiwa upandikizaji wa moyo kwa mafanikio.
WhatsApp Image 2025-07-31 at 14.56.32_ad7dbb4a.jpg
Imeelezwa kuwa mpango huo ni sehemu ya jitihada za JKCI katika kuimarisha huduma za kitaifa za moyo, kupunguza rufaa za nje ya nchi, na kuifanya taasisi hiyo kuwa kitovu cha huduma za moyo kwa kanda ya Afrika Mashariki.

Maadhimisho ya miaka 10 ya JKCI yanatarajiwa kuambatana na matukio mbalimbali ya kitaaluma, utafiti, huduma za kijamii, pamoja na uzinduzi wa mikakati mipya ya kuboresha huduma za moyo nchini.
 
Hiyo mioyo ya kupandikiza watakuwa wanaivuna Toka wapi,by the hongera kwao
 
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeanza rasmi maandalizi ya kuanzisha huduma ya upandikizaji wa moyo, hatua hiyo imeelezwa kuwa inatarajiwa kuendelea kuiweka Tanzania kwenye ramani ya huduma za juu za moyo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza Julai 30, 2025 kuelekea maadhimisho ya Miaka 10 ya JKCI, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Dkt. Peter *******, alisema kuwa mchakato huo ni wa kihistoria na utafungua ukurasa mpya katika utoaji wa huduma za matibabu ya moyo nchini.
"Tayari tumezindua Kamati Maalum ya Upandikizaji wa Moyo itakayosimamia maandalizi yote ya kitaalamu, kisheria na kiutendaji ndani ya kipindi cha miaka mitano. Hii ni hatua kubwa kwa nchi yetu na pia kwa nchi jirani ambazo hazina huduma hii," alisema Dkt. *******.

Aidha alifafanua kuwa huduma hiyo ya upandikizaji wa moyo inahitaji mchakato kwa kuwa yanatakiwa maandalizi makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji wa vifaa tiba vya kisasa, mafunzo ya wataalamu, pamoja na utaratibu wa kisheria na kimaadili.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Upandikizaji wa Moyo, Dkt. Evarist Nyawawa, alieleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utafuata mifumo bora ya kimataifa na kwamba tayari kuna takwimu zinaonesha kuwa watu zaidi ya 50,000 duniani wamekwishafanyiwa upandikizaji wa moyo kwa mafanikio.
Imeelezwa kuwa mpango huo ni sehemu ya jitihada za JKCI katika kuimarisha huduma za kitaifa za moyo, kupunguza rufaa za nje ya nchi, na kuifanya taasisi hiyo kuwa kitovu cha huduma za moyo kwa kanda ya Afrika Mashariki.

Maadhimisho ya miaka 10 ya JKCI yanatarajiwa kuambatana na matukio mbalimbali ya kitaaluma, utafiti, huduma za kijamii, pamoja na uzinduzi wa mikakati mipya ya kuboresha huduma za moyo nchini.
Pumbavu hawana ubavu wa kufanya hayo, pumbavu. Wanachoweza ni uchawa na kuiba kura......
 
Back
Top Bottom