Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imetangaza kutoa matibabu bure ya moyo kwa Wasanii wa Tanzania

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imetangaza kutoa matibabu bure ya moyo kwa Wasanii wa Tanzania

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imetangaza huduma ya kuwapima moyo na kuwapa matibabu bure Wasanii wa Tanzania ili kuwasaidia kuokoa maisha yao.

Akiongea leo December 13,2024 Mkurugenzi wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge amesema wametoa huduma hiyo kwa ajili ya kuokoa Wasanii wengi wanaopata maradhi moyo na kushindwa kupima mapema hivyo kubaini wanaugua kwa kuchelewa na kupelekea gharama za matibabu kuwa kubwa au hata kuhatarisha maisha yao.

“Mh. Rais ametutaka tuwafikie Wasanii na Watu mbalimbali kwa kuwapima kwa punguzo na tumeamua katika Clinic yetu ile ambayo ipo pale Kawe siku za Jumamosi na Jumapili tutatoa matibabu bure kwa Wasanii, bure unakuja unapimwa unachekiwa ili kugundua kama una shida, afya ndio kitu cha msingi, hatutaki tusikie Msanii ameanguka akiwa anaimba hatutaki, tukigundua una shida ya afya tunakuambia ufanye hivi na hivi na lakini Wasanii ni kioo cha Jamii mtatusaidia kuwaeleza Watu kuhusu magonjwa haya yasiyoambukiza”

“Nawaomba Wasanii mjiunge na Vyama vya Wasanii mkishajiunga tutawasiliana na Viongozi watawapa kadi maalum ambazo mkizitumia mtakuwa mnapata punguzo la bei, kuna wengine hawana bima kwahiyo inakuwa rahisi, ila tumieni siku za Jumamosi na Jumapili kupima bure na kupata matibabu bure”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Mamw Ongea na Mwanao, Steve Nyerere akiongea kwa niaba ya Wasanii ameushukuru Uongozi wa Muhimbili pamoja na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kujua umuhimu wa Wasanii wa Filamu na kuamua kuwashika mikono kwenye kuokoa maisha yao “Sisi tunapima vinywaji tu vinavyolewesha, vinavyoongeza nguvu za kiume lakini kupima moyo na kupima afya tunashindwa, tunapoteza nguvu kazi ya Taifa, kujigundua afya sio kufa inasaidia kuishi kwa umakini”
View attachment 3176200
Wako mamillioni ya watanzania hawana hela za matitabu. Nyie mna focus kwa wasanii! Ubaguzi huo!
 
Kuendelea kupata vichekesho vingine kutoka serikalini
Tuma neno Mi 5 tena kwenda namba (SA100)
 
Back
Top Bottom