Makanyaga
Platinum Member
- Sep 28, 2007
- 11,811
- 7,561
Iwapo wagonjwa hao wangetibiwa nje ya nchi, serikali ingetumia zaidi ya Sh. bilioni 178 kulipia gharama za matibabu hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi, alisema hayo jana wakati akielezea mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya tano kwa upande wa matibabu ya moyo, katika kikao cha Bodi ya Wadhamani ya taasisi hiyo.
Prof. Janabi alisema kwa wagonjwa hao kutibiwa nchini matibabu yao yamegharimu cha Sh. bilioni 89 fedha ambazo zimelipwa kupitia bima zao za matibu, misaada ya wafadhili mbalimbali wa nje, wagonjwa wenyewe kujilipia na serikali kugharamia matibabu ya wagonjwa wasio na uwezo wa kumudu gharama hizo.
“Gharama ya mgonjwa mmoja aliyefanyiwa upasuaji nje ya nchi ni zaidi ya Sh. milioni 30. Lakini kwa mgonjwa mmoja kutibiwa hapa nchini gharama zake hazizidi Sh. milioni 15.
‘Kwa kutibiwa hapa nchini fedha anazolipa mgonjwa zinatumika kununua vifaa tunavyomwekea katika moyo wake kama vile ‘pacemaker’, ‘high power device’, ‘stent’, ‘device closure’ na valvu. Vifaa hivi tunaviagiza nje ya nchi kwani havipatikani nchini”, alisema Prof. Janabi.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kwa kipindi cha miaka minne, wamewaona wagonjwa 300,836 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na nchi jirani kama vile Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Malawi, Ethiopia, Zambia, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Visiwa vya Comoro.
“Jambo la kufurahia ni kuwa tumefanikiwa kuokoa maisha ya watu ambao tumewatibu na hivi sasa wanaendelea na majukumu yao ya kazi za kila siku. Kwa kipindi cha miaka minne tulilaza wagonjwa 14,960, tumefanya upasuaji wa bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa wagonjwa 4,207 na upasuaji wa kufungua kifua na kusimamisha moyo kwa wagonjwa 1,747,” alisema.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambayo inamaliza muda wake Prof. William Mahalu, aliupongeza uongozi wa taasisi hiyo pamoja na wafanyakazi kutokana na huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa kwa wagonjwa wanaowatibu.
Prof. Mahalu ambaye ni mmoja wa madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa kwanza nchini, alisema anamaliza muda wa mwenyekiti wa bodi hiyo huku ndoto yake ya kuona Tanzania inakuwa na hospitali ya matibabu ya moyo ikiwa imetimia.
Chanzo: Nipashe