Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR): Asilimia 70 ya Saratani yabainika kwa Wanawake

Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR): Asilimia 70 ya Saratani yabainika kwa Wanawake

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imesema mzigo wa magonjwa ya saratani upo kwa wanawake kwa asilimia 70.

Pia imesema hakuna takwimu za kuthibitisha Kanda ya Ziwa inaongoza kwa matukio ya saratani nchini.

Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Yunus Mgaya, alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Kanda ya Ziwa kuongoza kwa matukio mengi ya saratani kuliko maeneo mengine.

“Tulichoona ni kwamba saratani inayoongoza kupitia takwimu hizo ni ya shingo ya kizazi kwa asilimia 37.5 kwa saratani zilizoripotiwa Ocean Road, saratani ya matiti asilimia 11,” alisema.

Aidha, alisema walipokea maagizo na kufanyia kazi kutoka Wizara ya Afya kutokana na taarifa zilizomfikia Rais kwamba Kanda ya Ziwa kuna matukio mengi ya saratani kuliko maeneo mengine.

“Tumepokea maagizo ya Wizara na tukashirikiana na taasisi mbili ya Ocean Road na Bugando, walikuwa na data za miaka mingi tuliamua kuchukua data ya miaka mitano kuanzia 2015 hadi 2019,” alisema.

Alibainisha kuwa kwa taasisi ya Ocean Road matukio ya saratani mbalimbali 16,546 na Bugando kulikuwa na matukio 4,562.

“Huu ni utafiti wa awali kujua ukubwa wa tatizo la kansa Tanzania, tumeangalia matukio haya kwa watu 100,000 kwa kutumia sensa ya mwaka 2012,” alisema.

Alieleza kuwa matokeo yalionesha kuwa kati ya watu 100, 000 kwa mkoa wa Mwanza, watu 19 wana saratani.

“Mkoa unaongoza kitaifa ni Dar es salaam watu 20, Pwani 15, Iringa 11.6, Kilimanjaro 11.2, Mara 10.2, Shinyanga 8, Simiyu 5, Tanga 12,” alifafanua.

Aidha alisema: “Ukichukua takwimu za Bugando kwa mikoa ya kanda ya ziwa, Mwanza inaongoza inafuatiwa na Mara, Shinyanga, Kagera, Geita, Simiyu.”

Kutokana na hilo, Mkurugenzi huyo alisema utafiti mwingine wanaotarajia kufanya hivi sasa na utakuwa wa muda mrefu ni kuangalia visababishi kwa watu hao wa saratani.

“Utafiti utaangalia mtindo wa maisha vikiwamo vyakula wanavyokula, shughuli wanazofanya kwa awamu ya kwanza picha tumepata visababishi kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa kimkoa kwa mikoa ya Mwanza na Geita ni saratani ya kibofu cha mkojo ambayo inasababishwa na kuwapo kwa kichocho kwa muda mrefu,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alitaka taasisi hiyo kwa kushirikiana na zile zinazohudumia wagonjwa wa saratani kushirikiana kutoa elimu kwa wabunge ili kuelewa ukubwa wa tatizo hilo na kuishauri Serikali.

Chanzo: IPP Media
 
Hakuna kitakachofanyika Tanzania kwasasa bila kupata reference ya Kanda ya Ziwa.
 
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba, alitaka taasisi hiyo kwa kushirikiana na zile zinazohudumia wagonjwa wa saratani kushirikiana kutoa elimu kwa wabunge ili kuelewa ukubwa wa tatizo hilo na kuishauri Serikali.

Kwanini asiombe hizo taasisi zitoe elimu kwa wananchi jinsi ya kufanya ili wasiweze kupata huo ugonjwa tishio au anataka kutengeneza mazingira ya posho??

Maana waathirika wakubwa ni wananchi na gharama za kujitibu ni aghali sana sasa hao wabunge wanataka kuishauri nini serikali wakati hizo taasisi zinatoa taarifa serikalini?

Hapo wapiganie tu elimu kwa wananchi hasa kwa hiyo mikoa yenye idadi kubwa ya wagonjwa
 
Hatuwezi kusema hivyo kwa sasa kwani ripoti hiyo aliyouitoa prof.yunus ni majumuisho tu ya tafiti mbalimbali za awali.

Pia isitoshe ukimsikikiza kwa makin prof yunus katika majibu yake na majibu aliyoyatoa Dr. Nestory Masalu ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Saratani Hospitali ya Rufaa ya Bugando, utabaini kuna harufu ya politics ndani yake.

Ndio maana naamini Labda tusubiri huo utafiti mpya wa sasa ambao utajumuisha wataalam mbalimbali na wengi zaidi kutoka nchi nzima. Ila kwa sasa tayari kuna kukinzana kikubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi tukisema kwamba saratani kwa wanawake zinaletwa na mabeberu? Sidiria nyingine zinakutwa na vitu vya ajabu kwenye uelekeo wa chuchu, pedi nazo kila kampuni inaweka vikorokoro vya ajabu mwisho wa siku madhara ni kwenye shingo ya kizazi.
 
Napendekeza watazame na jinsi ya kuleta tiba bora na sio mionzi..maana kilichotokea kwa kubadilika kwa seli au chromosome kirekebishwe na kwa kukarabati seli au chromosome na sio hiyo mionzi.
 
Back
Top Bottom