Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) yasema Wagonjwa 40 watabadilishwa nyonga

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) yasema Wagonjwa 40 watabadilishwa nyonga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Prof. Abel Makubi amewapokea madaktari bingwa wabobezi wa upasuaji wa nyonga Watatu kutoka nchi ya Pakistan watakaoendesha kambi ya siku tano ya upasuaji wa nyonga kwa wagonjwa 40 kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa MOI.
WhatsApp Image 2024-02-27 at 09.22.10_67ee4636.jpg

WhatsApp Image 2024-02-27 at 09.22.23_c5a9ce49.jpg
Katika kambi hiyo iliyoanza jana Februari, 26, 2024 jumla ya wagonjwa 40 wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha nyonga ambapo pia itatumika kama sehemu ya kuwajengea uwezo wa umahiri madaktari wazawa.

“Nashukuru kwa kuja kwenu, mjisikie mko nyumbani na iwapo mtapata changamoto yeyote msisite kuwasiliana nasi, uwepo wenu hapa ni wa umuhimu kwetu, tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu muhimu kwa ustawi wa maendeleo ya tiba hapa MOI” amesema Prof. Makubi

Kwa upande wake kiongozi wa wataalam hao kutoka Pakistan Abdullah Amjad ameushukuru uongozi wa MOI kwa mapokezi mazuri, ukarimu na ushirikiano walioupata.

“Tunashukuru kwa mapokezi mazuri, na tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri” amesema Amjad

Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Mifupa, Nyonga na Magoti Dkt. Athony Assey amesema kambi hiyo imeanza kwa upasuaji wa wagongwa wawili na baadae kuendelea na wengine hadi Machi, 01, 2024 kambi hiyo itakapomalizika.

Kambi hii ni matokeo ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita baada ya kuiwezesha MOI kuwa na vipandikizi vyakutosha (Implants) ambapo hapo awali wagonjwa walisubiri huduma hii muda mrefu kutokana na uhaba wa vifaa.
 
Hongera Serikali kwa maboresho mengi ktk sekta ya afya licha ya changamoto za hapa na pale.

Taasisi ya mifupa MOI ni taasisi yenye mapana ktk utoaji tiba kwa kuzingatia takwimu za ajali,magonjwa mtambuka yanayohitaji specialised treatment..Hivyo eneo na miundombinu ya sasa bado ni finyu lichs ya uwekezaji mkubwa na upanuzi.

Nashauri kutengwe eneo kubwa la ekari 25 mpaka 100 nje ya jiji kisha ijengwe Hospitali kubwa ya kisasa yenye huduma na vitendea kazi vya kisasa.

Gharama za matibabu MOI ni kubwa sana kwa sasa na Watanzania walio wengi wanashindwa kumudu ama kuzimudu kwa mahangaiko makubwa..Upo utaratibu wa kusamehe wagonjwa wasio na uwezo -HONGERA KWA SERIKALI YETU.

Tatizo ni hizi taasisi za Afya Muhimbili ikiwemo ni kuelemewa na madeni ya wazabuni na kupekelea huduma kuzorota..Ktk hili nadhani kunapaswa kuwa na namna sahihi ya Serikali kuongeza fungu la fedha la kulipia misamaha inayotolewa kwa wagonjwa,ndugu wa wafu wasio na uwezo mara baada ya kuhudumiwa.

Mungu ibariki Tanganyika,Zanzibar na JMT
 
Back
Top Bottom