The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Taasisi ya uhamasishaji uwazi na uwajibijaki katika rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) imetoa mafunzo maalum ya kuelimisha wananchi wasioona kuhusu ripoti na matumizi ya takwimu zinazotolewa na taasisi hiyo ili kuweza kuhoji na kufahamu mchango wa rasilimali hizo na fursa zilizopo kwenye sekta hiyo
Erick Katagory ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati (TEITI) amesema hadi kufikia mwaka 2025 ni zaidi ya nchi 57 Duniani zenye utajiri wa RasilimaliMadini, Mafuta na gesi asilia zimejiunga katika asasi ya TEITI, kati ya nchi hizo nchi 28 zinatoka Bara la Afrika ikiwepo Tanzania.
Katagory amesema madhumuni ya kujiunga katika asasi hiyo ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na uwazi katika matumizi ya Rasilimali Madini, Mafuta na gesi asilia ili kuboresha mapato na manufaa yatokanayo na shughuli za utafutaji, uchimbaji na biashara katika rasilimali hizo hapa nchini
kwa upande wake Mwenyekiti chama cha Wasioona Mkoa wa Dodoma Omari Lubuva ameishukuru Taasisi hiyo (TEITI) kwa kuwaandalia mafunzo hayo kwa watu wenye mahitaji maalumu
"Ni nadra sana kwa wakati kama huu kuona makundi kama haya yetu yanazingatiwa au kuonekana kama na sisi ni sehemu ya watu wanaotakiwa kupata taarifa ya kinachoendelea katika nchi yetu mara nyingi tumekuwa tukisahaulika"