Taasisi yetu mpaka sasa hakuna aliyepewa barua ya kupandishwa daraja

Taasisi yetu mpaka sasa hakuna aliyepewa barua ya kupandishwa daraja

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Ofisi yetu ina jumla ya watumishi wapatao elfu moja Tanzania mzima kwa makadirio.

Mpaka sasa kila nikiwapigia watumishi wenzangu walioko mikoa tofauti naambiwa hakuna aliyepata barua ya kupandishwa daraja au cheo.

Wiki mbili zilizopita tulijazishwa ma Opras. Wengine huyaita hopeless. Mimi miaka karibu yote nakataa kuyajaza, nimejaza majuzi baada ya kuambiwa kuwa yatawekwa mezani kusort watumishi watakaopanda madaraja.

Niko tayari kutoa ushirikiano kwa kuitaja ofisi husika endapo atatokea kiongozi kwa maelezo zaidi.
 
Yaani mko Elfu Moja afu ukashindwa kutaja hiyo taasisi?

Hii haki unaitafutaje kwa mafumbo hivyo?
 
Taja tu hiyo taasisi ili mjadala unoge.

Taasisi yako ni mfano tu ila ziko nyingi ambazo hazitaki kuweka wazi haya mambo ya promotion.

Serikali iagize lila taasisi iweke wazi orodha ya watumishi wanaotarajiwa kupanda cheo vinginevyo kuna watakaokuja kuachwa na malalamiko yataibuka na kuelekezwa kwa serikali kumbe tatizo ni Maafisa Utumishi.
 
Kutoa barua fake itakuwa ni kosa juu ya kosa na hawawezi kuthubutu.
Hawa watu nilishawahi kuwabananisha na Waziri mkuu Majaliwa.
Sasa hapa siwezi kuingia kichwakichwa maana wakijua ni mimi tena nimewachomekea watanitengenezea zengwe.
 
Kwa utaratibu wa sasa hupewi barua hadi mshahara ubadilike ili usije kudai malimbikizo. Baada ya payroll au mshahara kutoka na mabadiliko ndo unapewa barua
Sasa huoni kuwa huo ni uhuni.

Endapo hakuna atakayepanda daraja nchi yote huoni kuwa serikali itaendelea kujizolea ujiko kuwa wamewapandisha watumishi madaraja huku hamna kitu?

Kuna Taasisi wamewapa watumishi wao barua za kupanda madaraja je, wametenda kosa?
 
Watumishi walioingizwa mapema kwenye mfumo wengi wameshakuwa approved na hiyo imewafanya baadhi ya Taasisi kutoa barua kwa kuwa wana uhakika mshahara utabadilika na wengine wamesubiri hadi mshahara utoke ndo watoe barua.

Kuhusu kupandisha watu kama mtu ana sifa wengi watapanda mwezi na wachache watakaochelewa watapanda mwezi ujao. Kwenye hilo lazima tushukuru watu wamesota muda mrefu
 
Kidogo maelezo yako yamenituliza munkari kwa 65%
Watumishi walioingizwa mapema kwenye mfumo wengi wameshakuwa approved na hiyo imewafanya baadhi ya Taasisi kutoa barua kwa kuwa wana uhakika mshahara utabadilika na wengine wamesubiri hadi mshahara utoke ndo watoe barua. Kuhusu kupandisha watu kama mtu ana sifa wengi watapanda mwezi na wachache watakaochelewa watapanda mwezi ujao. Kwenye hilo lazima tushukuru watu wamesota muda mrefu
 
Sasa huoni kuwa huo ni uhuni.
Endapo hakuna atakayepanda daraja nchi yote huoni kuwa serikali itaendelea kujizolea ujiko kuwa wamewapandisha watumishi madaraja huku hamna kitu?
Kuna Taasisi wamewapa watumishi wao barua za kupanda madaraja je, wametenda kosa?

Nenda kwa HR wako aangalie status ya upandishwaji wako kwenye mfumo
 
Ofisi yetu ina jumla ya watumishi wapatao elfu moja Tanzania mzima kwa makadirio.

Mpaka sasa kila nikiwapigia watumishi wenzangu walioko mikoa tofauti naambiwa hakuna aliyepata barua ya kupandishwa daraja au cheo.

Wiki mbili zilizopita tulijazishwa ma Opras. Wengine huyaita hopeless. Mimi miaka karibu yote nakataa kuyajaza, nimejaza majuzi baada ya kuambiwa kuwa yatawekwa mezani kusort watumishi watakaopanda madaraja.

Niko tayari kutoa ushirikiano kwa kuitaja ofisi husika endapo atatokea kiongozi kwa maelezo zaidi.
Si usubiri tu itafika

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom