Ofisi nyingi hasa zilizo chini ya TAMISEMI ,watumishi waliombwa oprass hadi za miaka ya nyuma. Wengine walikuwa hawana, wakaanza kufoji kwa umakini hasa kipengele cha tarehe.
Sina uhakika, ila inasemekana walikuwa wana-upload font page na back page ambayo huwa ina comment, nafikir wajazaji wa oprass wanafahamu.
Umesema ulikuwa unapuuza kujaza oprass. Siku nyingine, hata kama unaona jambo halina umuhimu kwako, ila kama umeagizwa na kiongozi kulifanya, basi wewe lifanye tu.
Wakati mwingine viongozi wanaamua kutafuta sababu za kupunguza watu fulani kwa kuweka vigezo, ambavyo vinaweza kukuathiri kutokana na kupuuza. Kwa mfano, oprass zinatakiwa kukamilishwa mwisho wa mwaka. Sasa kama mlijaza kwa presha wiki mbili zilizopita, halafu mkajikuta mmezikosea (mfano kuback date), wakigoma kuwapandisha daraja, je utamlalamikia nani?
Ieleweke mpaka sasa, kigezo kimojawapo cha kupanda daraja ni oprass. Suala kwamba hawaziangalii, hilo ni wao. Ila wanaweza kuzifanyia kazi kisawa sawa. Hivyo, usiishi kwa mazoea!
NB. Mmejaza oprass wiki mbili zilizopita. Leo ni mwaka 2021, na mwaka haujaisha. Oprass zilizokuwa zinaangaliwa zaidi ni 2020 kushuka chini. Sasa nyie mmejaza oprass za lini?