Taasisi za dini hasa za Kikristo zipo kibiashara zaidi

FIKRA HAI

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
231
Reaction score
79
Imani ni jambo ambalo hupaswi kuigiza au kuingiza siasa ndani yake. Zaidi ni ukweli wa kiimani unajengwa ndani ya roho kwakuamini bila kuwekwa ushahidi wa dhahiri juu ya Hilo.

Ukienda kanisani siku ya Jumapili, utakutana na msululu wa michango kwa mwanajumuiya na harambee ambazo wengine wamefikia kuziita Simba na Yanga lengo kuu likuwa kuwanyonya Hawa waumini kwa kiwango Cha juu kabisa.

Katika harambee na michango hiyo utakuta Kuna ujenzi wa Shule ya seminari na waumini watachangia kwa nguvu zao zote.

Ni bahati mbaya shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za waumini hao kutowatambua watoto wa wajenzi hao waliojitoa kwa nguvu zao zote wakati wa ujenzi.

Shule hizo zinaendeshwa kibiashara na faida hiyo hairudishwi kwa waumini hao na hata kushindwa kutambua michango ya waumini hao katika kuzijenga.

Hakuna tofauti ya aliyejitolea na mtu asiyeshiriki katika ujenzi wa Shule, kwani wote hulipa kiwango sawa.
Huku ni kukosa uungwana na upendo unaohubiriwa makanisani.
 
Acha ku attack dini au mani za Watu Mkuu. We kama umeona kuna biashara sio sehemu zote, baadhi ya makanisa ndo kuna biashara ila sio wote
 
Kajenge yako mkuu utoe huduma zote bure gharama za kuendesha ziwe zako ndo utajua hajui kwanini mbuzi ana mkia mfupi.
 
Imani ni jambo ambalo hupaswi kuigiza au kuingiza siasa ndani yake. Zaidi ni ukweli wa kiimani unajengwa ndani ya roho kwakuamini bila kuwekwa ushahidi wa dhahiri juu ya Hilo.

Ukienda kanisani siku ya Jumapili, utakutana na msululu wa michango kwa mwanajumuiya na harambee ambazo wengine wamefikia kuziita Simba na Yanga lengo kuu likuwa kuwanyonya Hawa waumini kwa kiwango Cha juu kabisa.

Katika harambee na michango hiyo utakuta Kuna ujenzi wa Shule ya seminari na waumini watachangia kwa nguvu zao zote.

Ni bahati mbaya shule hiyo iliyojengwa kwa nguvu za waumini hao kutowatambua watoto wa wajenzi hao waliojitoa kwa nguvu zao zote wakati wa ujenzi.

Shule hizo zinaendeshwa kibiashara na faida hiyo hairudishwi kwa waumini hao na hata kushindwa kutambua michango ya waumini hao katika kuzijenga.

Hakuna tofauti ya aliyejitolea na mtu asiyeshiriki katika ujenzi wa Shule, kwani wote hulipa kiwango sawa.
Huku ni kukosa uungwana na upendo unaohubiriwa makanisani.
Hoja yako ina mantiki ndani yake.
 
Ingetakiwa waumin wao walio changia mtoto wake apewe ruzuku yaan asilimia fulan ya ada anasamehewa
Halafu hiyo faida hatujui inaenda wap??

Huu ni uhuni
 
Back
Top Bottom