Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Kutokana na mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknologia, Kumekuwa na changamoto kubwa sana kwa vijana wa kike na kiume kupata wenza sahihi wa kuoa/kuolewa na kwa wakati sahihi; Hii ni kutokana na mfumo mzima wa Elimu nk
Nashauri Makanisa na Misikini ianzishe utaratibu rafiki (wa faragha) ambao utaweza kuwakutanisha Vijana ( wa kike na kiume) ambapo Kijana atafika kwa wazee wa kanisa/Msikiti (kwa wakati wake) huku ameandika sifa za Msichana/Mume anayetamani kuwa naye;
Mfano kijana wa Kiume ataandika;
Vile vile wasichana wapate nafasi kama hiyo
Baada ya hapo wazee wa Kanisa/Msikiti watakaa na kupitia maombi ya pande mbili na kuanza kuona yanayo endana na kuwa kutanisha (faragha) kuona kama wataendana/watakubaliana.
Tunaweza kuta tunapata Ndoa bora na Imara kuliko nyingi za sasa hivi!!!
Hii haibadilishi utaratibu ulioko sasa hivi; Kijana atachagua mwenyewe njia anayo ona ni njema kwake !

- Majina yake kamili
- Anakaa wapi - akiambatanisha na copy ya kitambulisho chake cha taifa
- Ameoa au alishawahi kuoa? (kwa waislam kutakuwa na nyongeza, mke wa ngapi?
- Makazi (ananyumba, amepanga, anaishi kwa ndugu, anaishi kwa wazazi nk)
- Majina na mawasiliano ya ndugu yake angalau mmoja (yaweza kuwa mzazi) nk
- Anajishughulisha na nini na wastani wa kipato chake kwa mwezi
- Sifa za anayemtaka (sifa ataandika mwenyewe)
- Huu ni mfano tu ila Vigezo vinaweza kupangwa vizuri