Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Baadhi ya Taasisi za Serikali zilizopo wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro ikiwemo Jeshi la Polisi Hai, Shule ya Sekondari Hai Day zimetajwa kuwa na deni sugu la bili za maji inayofikia Zaidi ya Shilingi milioni 30 hali ambayo inawapa changamoto yakifedha na uendeshaji bodi ya Maji Uroki Bomang’ombe wilayani humo.
Amebainisha hayo leo Jumatano March 19, 2025 Afisa uhusiano wa Bodi ya Maji Hai Uroki Bomang’ombe Hardson Kimaro wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za Maji wilayani humo zinazofanywa na Bodi hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Hassan Bomboko wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Maji 2025 kwa wilaya ya Hai.
Amesema mamlaka hiyo imekuwa ikipambana na madeni sugu hasa kwenye taasisi zilizopo chini ya Serikali ikiwemo Polisi Hai ambao wanadaiwa kiasi cha Shilingi milioni 29, Shule ya Sekondari Hai day ambao wanadaiwa Shilingi milioni 8.8 mpaka kufikia mwezi February 2025.