Taasisi za Umma, Polisi na watumishi wa Umma mmefanya kosa gani hadi mfunge sehemu ya comments?

Taasisi za Umma, Polisi na watumishi wa Umma mmefanya kosa gani hadi mfunge sehemu ya comments?

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wakuu,

Teknolojia imeleta mabadiliko makubwa sana ikiwemo kwenye mawasiliano ikiwemo Web 2 ambayo inarahisisha watu kuchangamana na kutoa maoni yao katika mambo kadha wa kadha.

Kupitia maendeleo haya tunategemea kuona wananchi wakitoa maoni yao kwa uhuru na kushiriki katika mijadala mbalimbali huko mitandaoni.

Tulitakiwa kuamini kuwa teknolojia hii ingeweza kurahisisha ukusanyaji wa maoni ya wananchi na mtazamo wao juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea nchini mwao, taasisi za serikali, wasemaji na jeshi la polisi ambao moja kwa moja wanawajibika kwa wananchi wanakuwa wa kwanza kufunga sehemu ya kutolea maoni 'comment' section.

Sasa mnampostia nani kama hamtaki maoni? Si mkae nazo makwenu hizo taarifa? Na ni kipi haswa mnachohofia kutoka kwa wananchi? Mmefanya jambo gani baya hadi muwe na hofu hivi?

Huu hapa chini ni mfano kutoka kwwnye ukurasa wa jeshi la Polisi na walikuwa wanazungumzia ziara tu.
Screenshot_20250915-141451_Instagram.jpg
 
Wanajua wanachofanya sio sahihi na wabongo wamejawa nyongo wanatafuta pa kutemea
 
Waendelee kufunga hivyo hivyo hilo geshi lao Ra Porishi.

Siku wakijichanganya wafungue nitashuka nao jumla jumla mpaka page yao izimike.

Chezea spana za BICHWA KOMWE wewe!

Nagonga haswa. Ebo! Virungu kitu gani!
 
Back
Top Bottom