Taasisi za Serikali, mnapoweka mabanda kwenye maonesho kama Sabasaba na NaneNane, tafadhali hakikisheni mnaweka pia watu wanaoelewa vizuri taasisi na sekta mnayoonesha.
Hivi juzi nimepata fursa ya kutembelea maonesho ya Sabasaba na NaneNane, Dodoma na Dar es Salaam, kwa nyakati tofauti.
Nimetembelea mabanda ya taasisi kadhaa za Serikali takribani manne lakini changamoto niliyokutana nayo ni kwamba wakati mwingine unamkuta mhudumu ambaye ni mrembo au handsome na mwenye ustaarabu, lakini ukianza kumuuliza maswali ya msingi kuhusu taasisi yake, huduma, majukumu au sekta husika, majibu yanakuwa hafifu sana, hawazijui vema taasisi zao!
Hapo ndipo unajiuliza: hawaa?! Wameweka mtu kwa ajili ya kulipamba banda au kwa ajili ya kuiwakilisha taasisi na kuwapa wananchi huduma?
Hakuna tatizo kuwa na maafisa wa mapokezi, mawasiliano au PR kwenye mabanda.
Lakini ni muhimu waambatane na wataalamu wa sekta husika ambao wanaweza kueleza kwa usahihi sera, huduma, miradi, takwimu, changamoto na fursa zinazohusiana na taasisi.
Maonesho ni fursa kubwa ya kuelimisha umma, kujenga uelewa na kuonyesha thamani ya taasisi kwa wananchi.
Usipokuwa na mtu mwenye maarifa ya kutosha, unakuwa umepoteza sehemu kubwa ya fursa hiyo.
Taasisi za Serikali, wekeni watu wenye uelewa wa taasisi kwenye mabanda yenu.
Muonekano ni muhimu, lakini maarifa ndiyo yanayomfanya mgeni aondoke akiwa ameelewa kitu.
Wekeni watu wanaoijua taasisi husika vema.