Taasisi za Umma Wekeni Wataalamu Kwenye Mabanda ya Maonesho, hawa wengi Mnaotuwekea uwezo mdogo

Taasisi za Umma Wekeni Wataalamu Kwenye Mabanda ya Maonesho, hawa wengi Mnaotuwekea uwezo mdogo

Hapo wanalogana anataka kila event asafiri yeye apate hio perdiem na saa nyingine waandamiz unakuta wanaona sio ishu nenda ukapate wewe hio laki 6.
Ni shida sana mi nimekuwa naenda sana kwenye haya maonesho unakuta kila mara maafisa ni walewale ila bado mambo mengi yanayohusu huduma wanazotoa hawayajui vizuri tofauti na ukienda mabanda ya taasisi za binafsi sehemu ambayo niliridhika mara nyingi ni mabanda ya magereza na vyuo wanajitambua sana ila hawa mamlaka na wakala wajitathmini baadhi wanaleta mabandani watu viande!
 
Mkuu imeleta hoja nzuri sana,
Kwa kifupi hapo unaweza Kuta Kuna mambo kama haya.
✓ Mapenzi ndani ya ofisi, demu mzuri analiwa na mkuu wa idara Fulani, lazima apewe Mchongo ili nae akale perdiem

✓Uchawa, unakuta hao ndio machawa wa DED, CEO, DG, au Mkuu wa Kanda

✓ Ujuaji, wakiwa Ofisi wanajifanya wajuani sana kumbe ni vilaza tu

✓ Uchawi, Kuna watumishi wengi kazi ni kuwaloga wenzao wasionekane ili waonekane wao tu

✓ Unafiki, kusagia kunguni wenzao ili wao waonekane bora

✓ Bahati tu zinawabeba ukichagiwa na mionekano yao lakini kichwani hamna kitu
Yaani hapo umekamilisha...ukienda maoneshoni ni kama mashindano ya umiss_ wanasahau sisi hatuendi kuangalia sura za watu tunataka huduma - hizo figisu ni tatizo kwenye ofisi nyingi za umma inabidi mifumo mbali na iliyopo kama sijui ndio opras mnasema isaidie kuboresha utendaji na kuvunja majungu kwenye utumishi kuna siku nilimsikia mdau analalamika kuhusu watu kupewa kazi ambazo hawajasomea imekuwa tatizo sana huko kwenye baadhi ya public institutions
 
Taasisi za Serikali, mnapoweka mabanda kwenye maonesho kama Sabasaba na NaneNane, tafadhali hakikisheni mnaweka pia watu wanaoelewa vizuri taasisi na sekta mnayoonesha.

Hivi juzi nimepata fursa ya kutembelea maonesho ya Sabasaba na NaneNane, Dodoma na Dar es Salaam, kwa nyakati tofauti.

Nimetembelea mabanda ya taasisi kadhaa za Serikali takribani manne lakini changamoto niliyokutana nayo ni kwamba wakati mwingine unamkuta mhudumu ambaye ni mrembo au handsome na mwenye ustaarabu, lakini ukianza kumuuliza maswali ya msingi kuhusu taasisi yake, huduma, majukumu au sekta husika, majibu yanakuwa hafifu sana, hawazijui vema taasisi zao!

Hapo ndipo unajiuliza: hawaa?! Wameweka mtu kwa ajili ya kulipamba banda au kwa ajili ya kuiwakilisha taasisi na kuwapa wananchi huduma?

Hakuna tatizo kuwa na maafisa wa mapokezi, mawasiliano au PR kwenye mabanda.

Lakini ni muhimu waambatane na wataalamu wa sekta husika ambao wanaweza kueleza kwa usahihi sera, huduma, miradi, takwimu, changamoto na fursa zinazohusiana na taasisi.

Maonesho ni fursa kubwa ya kuelimisha umma, kujenga uelewa na kuonyesha thamani ya taasisi kwa wananchi.

Usipokuwa na mtu mwenye maarifa ya kutosha, unakuwa umepoteza sehemu kubwa ya fursa hiyo.

Taasisi za Serikali, wekeni watu wenye uelewa wa taasisi kwenye mabanda yenu.

Muonekano ni muhimu, lakini maarifa ndiyo yanayomfanya mgeni aondoke akiwa ameelewa kitu.

Wekeni watu wanaoijua taasisi husika vema.
Posho posho

Wakubwa wanapeleka watu wao wapate posho wanaacha watu wenye uwezo.
 
Back
Top Bottom