Taasisi za Umma Wekeni Wataalamu Kwenye Mabanda ya Maonesho, hawa wengi Mnaotuwekea uwezo mdogo

Hapo wanalogana anataka kila event asafiri yeye apate hio perdiem na saa nyingine waandamiz unakuta wanaona sio ishu nenda ukapate wewe hio laki 6.
Ni shida sana mi nimekuwa naenda sana kwenye haya maonesho unakuta kila mara maafisa ni walewale ila bado mambo mengi yanayohusu huduma wanazotoa hawayajui vizuri tofauti na ukienda mabanda ya taasisi za binafsi sehemu ambayo niliridhika mara nyingi ni mabanda ya magereza na vyuo wanajitambua sana ila hawa mamlaka na wakala wajitathmini baadhi wanaleta mabandani watu viande!
 
Yaani hapo umekamilisha...ukienda maoneshoni ni kama mashindano ya umiss_ wanasahau sisi hatuendi kuangalia sura za watu tunataka huduma - hizo figisu ni tatizo kwenye ofisi nyingi za umma inabidi mifumo mbali na iliyopo kama sijui ndio opras mnasema isaidie kuboresha utendaji na kuvunja majungu kwenye utumishi kuna siku nilimsikia mdau analalamika kuhusu watu kupewa kazi ambazo hawajasomea imekuwa tatizo sana huko kwenye baadhi ya public institutions
 
Posho posho

Wakubwa wanapeleka watu wao wapate posho wanaacha watu wenye uwezo.
 
Posho posho

Wakubwa wanapeleka watu wao wapate posho wanaacha watu wenye uwezo.
Ni tatizo sana...hili nalo lianze kusimamiwa waache kutuletea viande kwenye maonesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…