Taasisi zinazoongoza kwa Rushwa ndiyo Walinzi wa Haki

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Kwa mujibu wa katiba yetu hii yenye mapungufu mengi, wasimamizi wakuu wa sheiia ni Polisi, na chombo cha kutafsiri sheria hizo ni Mahakama.

Sheria ndiyo inayoonesha haki yako na isiyo yako. Kwa hiyo taasisi hizi mbili, Polisi na Mahakama ndiyo wasimamizi wa haki. Na hiyo ipo Duniani Kote.

Miaka yote ilipokuwa inatolewa taarifa juu ya ulaji Rushwa, wakati wote, kinara wa rushwa, kwa taasisi, aliyekuwa akiongoza ni POLISI akifuatiwa kwa ukaribu na MAHAKAMA.

Ni jambo la kufikirisha sana. Rushwa hupofusha macho. Humfanya mlaji rushwa asitende haki. Leo tuna Jeshi la Polisi, na Mahakama, vyote vyombo vya kusimamia haki, kwa taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa kila mwaka (ukiacha kipindi cha awamu ya 5), ndizo taasisi zinazoongoza kwa ulaji rushwa, yaani ni taasisi zinazoongoza kwa kupofuka macho kwa sababu ya rushwa (rushwa ya vyeo na rushwa ya pesa), lakini sisi wananchi tunasubiria kutendewa haki na taasisi hizi. Hivi sisi tuna akili? Huku siyo sawa na kusubiria samaki wadondoke toka kwenye mti wa mbuyu?

Mahakama na Jeshi la Polisi, taasisi hizi, ni kati ya taasisi zinazotakiwa kuundwa upya, ili kuziondoa kwenye mwelekeo wa ulaji rushwa na kuzipeleka kwenye mwelekeo wa utoaji haki.

Leo hii, ukiwa una haraka, unasafiri, uwe na kosa au huna kosa, kama unaendesha gari, unalazimika pembeni ulipokaa kuweka elfu tano tano au kumi kumi kwaajili ya polisi njiani maana bila hivyo, watakuchelewesha, watakuzungusha, na njiani ni wengi, huwezi kuwahi unakoenda. Wapo watakaokuomba moja kwa moja, wapo watakaokulazimisha kwa kukutafutia makosa.

Ukienda mahakamani, hali ni hiyo hiyo. Ndiyo maana kesi ikifika mahakama kuu, watu wanataka kujua kesi inasikilizwa na jaji gani. Hata hukumu ikitoka ili upate nakala ya hukumu haraka, ni lazima umtafutie chochote karani na jaji.

Jambo la kujiuliza, hivi vyombo viwili, ni vyombo vya utoaji haki au uvurugaji haki? Mara nyingi mahakama zetu zimetumika kama mihuri ya kuidhinisha uovu na dhuluma. Kuna wakati unaona wazi kabisa, ni aheri hata kwenye mabaraza ya koo kule vijijini yanahukumu kwa weledi kuliko wanaojiita majaji, na sababu kubwa ni kuwa wale wazee vijijini hawajui vifungu vya sheria lakini wanajua iliyo haki. Majaji wetu wengi wanatumia ujuzi wa vifungu vya sheria, kupindisha haki ili kufikia hukumu wanayoitaka wao na siyo ile inayotakiwa na haki.
 
Rushwa hukumu yake iwe kifo, ndio soln pekee vinginevyo hakuna suluhisho
 
Aisee rushwa na police ni kama samaki na maji huwezi watenganisha kabisa, police ndio vinara wa rushwa kilazima hichi chombo kimeoza kijichunguze
Yan polisi wetu Wana tia kinyaa Yan mpaka Raia wakigeni hawa wataki kuwaona Yan wazungu Wana sema polisi wetu wanapenda rushwa sana yani mpaka jinsi ya kuwa tetea polisi wetu tunashindwa Yani polisi walipo fikia hawa aminiki tena na wageni yani mzungu ana hiari aka ombe msaada kwa mlinzi wa kampuni binafsi kuliko kwenda kuuliza Jambo kwa polisi, Yani katika taasisi inayo ongoza kwa kuichafua nchi yetu kimataifa polisi wanaongoza.
 
Kuna wakati kulitokea wizi kwenye kampuni, kulikuwa na pendekezo toka polisi waweke kituo karibu ili wasaidie kulinda, wazungu walikataa kabisa. Sababu ilikuwa moja, kuwa wakiletwa polisi, wizi ndiyo utazidi.

Kwa sababu Polisi watatumika kuwalinda wezi. Ilionekana ni afadhali kuwatumia walinzi wa kampuni, japo kuna wakati wanazidiwa kukiwa na matukio makubwa ya ujambazi, lakini kuna unafuu kwa sababu matukio hayo hayawi mengi.

Kijijini kulikuwa na uhalifu mwingi. Nikapendekeza tujenge kituo cha polisi kisha tuombe kuwa na kituo kidogo cha polisi. Wananchi walikataa kabisa, na kusema hao polisi ni wadhulumaji wakubwa, kiasi ambacho ni aheri kuendelea kupambana na uhalifu huu mwingine kuliko uhalifu wa jeshi la polisi.
 
Taasisi zinazoongoza Kwa Rushwa ndogondogo za Kila siku ni Polisi, Tanesco, lakini Rushwa kubwakubwa za kifisadi ni Wizara ya Nishati, madini na wizara ya ujenzi. Humu Rushwa zao ni za kuuza nchi kabisa. Mabilioni, mfano escrow
 
Hivi huko kwenye mafunzo Yao huwa wanafundishwa kuchukua rushwa kilazima maana ma police wote nchi nzima wanatabia za kufanana ikifatiwa na uhamiaji, haya majeshi yajichunguze ikiwezekana wabadili mafunzo why chombo Cha kusimamia usalama kiongoze kwa rushwa?
Mbona walinzi binafsi huwa hawataki rushwa
 
Ni muhimu kuchunguza mitaala ya polisi ili kujua huwa wanafundishwa nini.

Maana karibia wote ni wala rushwa

Karibia wote wanapenda kuonea watu

Wapelelezi karibia wote cha kwanza wanachojua ni kumpiga mtuhumiwa

Karibia wote wanaona wana haki ya kuoewa fedha na watu wengine.
 
Hata kama unashauri Mahakamani na haki iko upande wako.. Ukitaka liishe ndani ya mwaka ni wewe tu.

Bila hivyo kesi inaweza kukaa miaka 5
Rushwa ni kitu kibaya sana
 
Ni muhimu kuchunguza mitaala ya polisi ili kujua huwa wanafundishwa nini...
Hili jeshi lijitafakari labda syblus zao zimepitwa na wakati, haiwezekani wote wawe na tabia za kufanana na kudai rushwa na hela kwa Raia kinguvu ukigoma wanakupa kesi hata ya mauaji, au kukuwekea madawa ya kulevya Ili ufungwe kifungo Cha maisha.

Jeshi linahitaji reformation kubwa
 
Yaani kuna mazingira mengi, maisha yangekuwa bora zaidi bila ya polisi.
 
Yaani kuna mazingira mengi, maisha yangekuwa bora zaidi bila ya polisi.
Yes hii nchi yetu swala la haki bado ni gumu sana, hao hao watoa haki Ili upate stahiki yako lazima uwahonge hela kwanza, inasikitisha sana
 
Hao viongozi wa juu mliwahi kuwazungumzia? Hao ndiyo walaji wakubwa wa rushwa! Let to feed this cake of nation!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…