Taasisi zote za Serikali zihamie Dodoma

moma2k

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2010
Posts
1,093
Reaction score
1,408
Wananchi toka mikoa ya pembezoni mwa nchi tunaumia sana kusafuri toka Sumbawanga, Kigoma, Kagera kwenda mpaka Dar es salaam kupata huduma kwenye taasisi za serikali.

Tunaomba wahamie haraka Dodoma. Ikulu na wizara zote zimeshahamia Dodoma. Wao wanasubiri nini?
 
Unateseka ukiwa wapi? Mbona taasisi zote zina presence dodoma?
 
Naunga mkono hoja 200%
 
Hivi na hii mikoa nayo huwa inahitaji huduma ya serikali?
 
HAKUNA SABABU WAKATI YAPO MA V8 MAPYA MAFUTA FULL TANK WACHA WAENDELEE KUWA DAR WALE RAHA NCHI TAJIRI SANA
 
Makosa makubwa sana kutumia trilions of money kuhamia Dodoma mji uko jangwani wakati hakukuwa na uharaka! TAZAMA BALOZI ZOTE ziko Dar na hazihamii Dodoma kwa sasa
 
Baadhi ya Wizara ziko hapa Dar es salaam,wiki sasa kwa ajili ya maonyesho ya Saba Saba. 🤔
 
Watahamia tu mkuu,kama mwenye nchi kashahamia unategemea nani atatia ngumu,ngoja zile ofisi ziishe kule Mtumba,nimesikia jana kuanzia mwezi October zitakuwa zimeisha...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…