Taazia: Dr. Tamim Bushiri

Taazia: Dr. Tamim Bushiri

So ikikaa kiimani inakuwa ni Siri?
Mkuu Azarel

Kiimani kama Kuna mtu alikuwa ni mdhambi(alitenda dhambi enzi za Uhai wake) ataanza kuadhibiwa tangu akiwa kaburini

Ukisoma [Ghaafir: 45 – 46].

Hiyo Aayah iko wazi kabisa kuwepo kwa adhabu ya kaburi kabla ya Siku ya Qiyaama.
 
Sasa vipi kama Mtu amefia baharini hajapata kuzikwa katika kaburi?
 
Lengo la hiyo Hadithi ni kutukumbusha kutenda mema na kuacha dhambi

Hata ukifia baharini/ukaunguzwa moto kama wezi wafanywavyo lakini still utayahisi hayo maumivu

Tutende mema Mkuu ili tupunguziwe adhabu ya kaburi 🙏
 
Mtu ameuguwa ujawai kwenda kumuona hosipitali leo kafariki unaibuka kumsifu
 
Poleni sana, Ila nimeshindwa kuelewa hapo kwa kaka yako Mgone, umeanza kumwita Dr. Mgone kisha chini ukamwita Prof. Mgone

Kipi ni sahihi? Unaweza kutupatia historia ya Ilmu yake?
Labda alimtambulisha kwake akiwa Dr. na sasa ni Prof. Najaribu kuwaza tu Mkuu
 
Ukitambua uwepo.wa imani za watu wengine hauwezi uliza swali la kipuuzi kama hili Mkuu.
Ni kwa vipi hilo swali ni la kipuuzi? Hebu punguza jazba

Kaburi nalifahamu, halina uhai...nikauliza adhabu ya kaburi ni ipi? Kaburi linaweza kuadhibu?

Wewe na kiherehere chako ambaye hujaukizwa unasema swali la kipuuzi, unawashwa?
 
Waislamu ndiyo wanajua kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao, ni kama nyie mnavyofundishwa kwamba hamna dhambi kwa sababu dhambi zenu zote zitakuwa zimefutwa na Yesu baada ya kusulubiwa.
Umewahi kusikia kuna Muislamu yeyote amehoji kuhusu jambo hilo? Kwa sababu yeye halimuhusu.
Kwani wakina mazinge wanaouchambua ukristo vipi unawahusu?
 
Ni kwa vipi hilo swali ni la kipuuzi? Hebu punguza jazba

Kaburi nalifahamu, halina uhai...nikauliza adhabu ya kaburi ni ipi? Kaburi linaweza kuadhibu?

Wewe na kiherehere chako ambaye hujaukizwa unasema swali la kipuuzi, unawashwa?
Unaijua theolojia ya waislamu juu ya kifo na kaburi?.
 
Poleni sana, Ila nimeshindwa kuelewa hapo kwa kaka yako Mgone, umeanza kumwita Dr. Mgone kisha chini ukamwita Prof. Mgone

Kipi ni sahihi? Unaweza kutupatia historia ya Ilmu yake?
Shukrani Kwa taarifa Mkuu sana Mohamed Said

Huenda nilisoma taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusu wawili hawa

Vipi kuhusu Oscar Kambona na Mwl Nyerere, Kipi kilitokea watu hawa wawili kugeuka maadaui baina yao licha ya nyakati kadhaa kufanya kazi pamoja huko nyuma?

Na kama hautajali unaweza kuelezea vile unavyofahamu sababu hasa ya Mwl Nyerere kufanyiwa majaribio kadhaa ya kutaka kupinduliwa na Jeshi? Mathalani niliwahi kusoma humu mtandaoni kuhusu jaribio la akina Zakaria Hanspope na wenzake kujaribu kumpindua..

Shida hasa ilikuwa ipi kutaka kufanikisha hilo?

View: https://youtu.be/Z8yCweRdqOk?si=17VymD_XQdsyV7LT
 
Mzee najua wajua

Upatapo muda ,tuweke sawa kuhusu namba 115 ,aliyotoka nayo shimoni ndg Forojo ganze ,huko bagamoyo na akina mzee yahaya hussein ,juu ya mwenge na asili yake
 
DR. TAMIM DAKTARI AMBAE HAKUGOMA MADAKTARI WALIPOGOMA

Nimempiga Dr. Tamim picha nyingi na zote ninazo zipo Maktaba.

Kila picha niliyompiga nilijitahidi kumpelekea nakala.

Tabu iliyonifika ni picha ipi nichague itakayomueleza na kumuonyesha yule ambae hakupata kumfahamu Dr. Tamim katika uhai wake alikuwa mtu wa aina gani.

Nimechagua picha hii Dr. Tamim amekaa kwenye kizingiti cha Msikiti wa Makonde.

Dr. Tamim amekaa kwenye kizingiti cha msikiti.

Ndani msikiti ulikuwa umejaa watu wanasalia maiti.

Ilibidi wengine wabakie nje.

Msikiti wa Makonde juu ya ukongwe na umaarufu wake si katika misikiti yenye nafasi ya kuchukua watu wengi.

Watu wangeamua kufunga safu hadi nje kusalia jeneza ingebidi Mtaa wa Swahili makutano na Msimbazi ufungwe kwa magari na wenda kwa miguu.

Hakuna asiyejua hekaheka ya magari ya kawaida, Mwendokasi, Bodaboda, Daladala katika makutano ya Swahili na Msimbazi.

Dr. Tamim Daktari Bingwa wa Watoto amekaa nje kwenye kizingiti cha msikiti akisubiri jeneza litoke tuelekee mazikoni.

Nimemjua Dr. Tamim tayari mganga yuko Makuti Clinic, Muhimbili akiwa pale na kaka yangu Dr. Mgone.

Kaka yangu ndiye aliyenijulisha kwake na tukawa marafiki ndugu.

Katika taarifa za msiba nilizopokea mapema moja ni kutoka kwa kaka yangu Prof. Mgone.

Hapa Makuti Clinic hapahitaji maelezo kwani baba, mama na watoto wao ambao sasa pengine na wao ni baba na mama hapa wanapajua vyema ama kwa wao kukumbuka kuambiwa na mama, "Ukiendelea na utundu wako nitakupeleka kwa Dr. Tamim akakuchome sindano."

Naamini leo wapo vijana waliokuwa wanatibiwa na Dr. Tamim Makuti Clinic watoto wao baadae wametibiwa na yeye.

Mgomo wa madaktari ulitikisa serikali.

Vyombo vya habari vikapata stori ya kuuza gazeti.

Asubuhi naangalia Daily News habari kuu iliyoandikwa kwa kichwa cha habari kwa wino mweusi uliokoza ni mgomo wa madaktari.

Chini ya kichwa cha habari naona picha ya Dr. Tamim yuko hospitali anatibia wagonjwa.

Dr. Tamim yeye hakugoma.

Nilipokutananae nikamuuliza kwa nini hakugoma?

"Mimi siwezi kugoma kwa sababu wako wale wagonjwa wametoka mbali sana mfano wa Chamazi kabadili mabasi hadi kafika Muhimbili akitegemea tiba.

Hawa ndiyo walionifanya mimi niende hospitali kuwasubiri niwatibu.

Wako wagonjwa nikiwa pale hospitali nawaona wanapoelezwa hakuna huduma wanaingia kwenye magari yao wanakwenda kwenye hospitali za kulipia.

Hawa si watu wa dhiki.

Lakini vipi jamaa zangu wa Manzese Uzuri hawa maskini ya Mungu watakwenda wapi wakinikuta mimi sipo?"

Huyu ndiye Dr. Tamim.

Watu wengi wamepita mikononi mwake kwa kutibiwa.

Aliwapenda watu na watu wakampenda.
Tamim hakuwa mtu wa kujikweza.

Tamim hakuwa mtu wa kujiona.

Tamim alikuwa mtu wa msaada kwa amjuaye na asiyemjua.

Buriani ndugu yetu.
Umeacha jina.

Wengi hawatakusahau.
Mwenyezi Mungu alipanue kaburi lako.

Amin.

Acha propaganda una lako jambo ww sio bure
 
Mzee wangu
Samahani Ni taazia au tanzia?

Apumzike kwa amani mzee wetu Tamimu
 
Mzee wangu
Samahani Ni taazia au tanzia

Apumzike kwa amani mzee wetu Tamimu
Dr....
Lugha inategemea na msemaji.
Mimi ni Mswahili hili na sina lugha nyingine mama ila Kiswahili.

Husema, "Khabari."
Si "Habari."

Ndiyo unaona, "Taazia" si "Tanzia."
Maneno yote ni sawa hakuna tatizo.
 
Back
Top Bottom