Tabia 4 za watu waliofanikiwa katika umri mdogo

Tabia 4 za watu waliofanikiwa katika umri mdogo

Mfukutuzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2015
Posts
239
Reaction score
175
TABIA 4 ZA WATU WALIOFANIKIWA KATIKA UMRI MDOGO

1. Zifuate nafasi za kufanikiwa zilipo, usikae ukisubiri zikufuate. Kama kilimo cha vitunguu ni Mbeya, wewe Dar hapakufai, nenda uone mambo yanaendaje. Kama dili za mawe ziko Geita na Arusha fuata zilipo. Kama elimu iko kwenye vyuo wewe mtaani panakuzingua tu. Elimu haitakufuata wala mali haikufuati. Mafanikio unayatafuta, hayakutafuti ndugu yangu.

2. Kuwa na mshauri mzuri. Mjomba, rafiki yake baba, boss wako, mfanyakazi mwenzako mwenye experience zaidi ya maisha, etc. Hawa watu huwa wameona mbali kabla yako na kama wako wazi katika mioyo yao basi watakupa walau mwanga wa jinsi ya kujipanga na mambo. Ukichukua mawazo yao ukachanganya na yako na mkono wa Mungu mambo safi.

3. Usiweke mayai yako yote katika kapu moja. Pambana huku na kule. Sawa unalipwa labda mshahara wa laki 6 kwa mwezi. Hata siku moja hizo akiba za laki laki hutaweza kuhama ulikopanga na kujenga kwako. Lakini hizo laki laki ukiziwekeza mahali baada ya miaka mitatu huku kazi inaendelea utakuwa tofauti. I am telling you!

4. Ziba masikio. Ukisikiliza sana ya watu hutafanya lolote kwenye maisha. Mara fulani yuko hivi mara yuko vile. Sio ishu. Wewe muamini Mungu wako na fanya yako. Watu wataongea tu haijalishi unafanya mazuri au mabaya so focus on your things na Mungu wako na mipango yako.
 
Kwa nchi yetu ilivyo hata ukiwa na sifa hizo hapo juu bado huwezi kufanikiwa katika umri mdogo labda uwe mwizi, malaya, au urithi mali kwa wazazi wenye uwezo otherwise huo ushauri utabakia tu kuwa ngonjera tu.
 
Nzuri hiyo mitaji na urasimu mkubwa wa akina kaisali unatutesa sisi walala hoi.
 
Nzuri hiyo mitaji na urasimu mkubwa wa akina kaisali unatutesa sisi walala hoi.

Kikubwa ni urasimu, kuna watu wao kazi yao kila kukicha wanapanga mipango ya kuwanyonya walio chini yao, lakini dawa tunayo, ni kuwatoa katika uongozi kwa silaha moja tu ambayo ni 'kura'
 
Kwa nchi yetu ilivyo hata ukiwa na sifa hizo hapo juu bado huwezi kufanikiwa katika umri mdogo labda uwe mwizi, malaya, au urithi mali kwa wazazi wenye uwezo otherwise huo ushauri utabakia tu kuwa ngonjera tu.

Usiwe na mawazo hayo my brother, kufanikiwa kunawezekana ikiwa tu hutadharau kazi, jifunze kwa Maganga ana miaka 27 ni muhitimu wa SUA, alianza kilimo akiwa mwanafunzi kwakushawishiwa na mtu kwa mtaji usiozidi mil 1.5 lakini leo hii anamiliki heka 76 za miti ya mbao na heka kadhaa za mashamba ya mazao ya muda mfupi, hakupewa urithi ili wala kuiba, alianza na kufuga kuku kisha akapata hicho kimtaji, jaribu kufikiri miaka 4 ijayo atakuwa wapi kujana huyu mdogo???? yote yanawezaka ikiwa mtu ataamua kuachana na kusubiri kuajiriwa.
 
Kikubwa nikusema naanza leo, uvivu unasumbua watu, kufanikiwa ni kupanga tu hebu tuseme mtu angeanza biashara au kilimo kwa lengo maalum 2010 leo angekua wapi? nadhani angekua anawaza makubwa.
kuna jamaa yangu mmoja mwaka 2000 alikuwa mgambo wa kusaka kodi na alikuwa mlevi wa gongo, kodi zilipo futwa maisha yakawa mabaya zaidi+na ulevi, akaamua kufanya vibarua na kuanza kilimo na akaacha pombe sasa ana maisha mazuri gongo haikumbuki tena
 
siri ya mafanikio katika hesabu rahisi na ya kawaida kabisa.
NJOZI(VISION) + IMANI + TENDA.
Wengi hukomea kwenye njozi na imani, kwa visingizo vya mtaji, mtaji hautoki angani, Mungu wetu huwalisha ndege wakati wote, hawalishi kwa kuwapelekea chakula viotani mwao. tukumbuke tu kuwa hatua mia huanzwa na moja. mtaji unaodhani ni tatizo, kumbuka elfu kumi inatosha kuwa mtaji, ni namna ulivyojianda. kwa kumsaidia kijana mmoja elfu kumi mwaka juzi, ilitosha kuwa mtaji kwa kijan huyo na sasa ana kibanda cha duka kikubwa sana. elfu kumi ilimfanya anunue brushi na dawa ya viatu, baada ya siku 3 akaja na kiti akakaa chini ya mti karibu na ofisi za Halmashauri moja, akitoa huduma ya kupiga dawa viatu vya wafanyakazi na wahitaji huduma katika halmashauri hiyo, hivi sasa, ni mtu mwingine kabisa.
 
Ni kweli ndugu, hapo umetoa mfano wa 10,000/= lakini huyu anayelalamika mtaji utakuta simu yenyewe anayotumia ni ya 150,000/= kwenda juu.

Vijana sasa tunaathiriwa na mambo mengi;
1. Kukimbizana na mabadiliko ya teknolojia (kutaka kila toleo jipya uwe nalo wewe)
2. Kubagua kazi (tumezoea kuonekana sisi ni wa type flani hivyo tutajidharirisha)
3. Tunadhani biashara mpaka ushike mabilioni ya pesa
 
Safi sana..hyo ya nne ndo watu wangi wanakoseaga..mtu anakuwa na ideal nzuri then anaanza kujiuliza nikifanya watu watanionaje..huu ni upumbavu uliopindukia..hii dunia hatupaswi kuangalia watu wanasema nn simamia kile unachokiamini,...
 
Back
Top Bottom