Tabia halisi za Mtanzania

Tabia halisi za Mtanzania

Tyrex

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2012
Posts
2,373
Reaction score
5,100
Tuorodheshe tabia za waTanzania halisi

1 Anakukopa hela kiupole ila ukidai automatically unakua mtu mbaya kwake asiyefaa

2 Kabla hajajua cheo chako au wadhifa wako anakutreat kama takataka ila akisikia wew mtu flan ghafla treatment inabadilika

3 Mkiwa mnamiadi maybe kuonana au mnaonana saa flan na ukamjulisha kabsa unatoka eneo ulipo huku akijua wew hujui maeneo alipo yeye unaweza shangaa unafika unapiga simu hapokei na baada ya masaa 2-4 akakwambia eti simu ilikua silent au alikua anapika n.k

4 ukipanda cheo au kumzidi kitu flan anachukia kabsa

5 Akisikia matatzo ya mwenzake anafurahi sana

6 Wanapenda kusaidiwa tu walio wengi na kuona msaada ni haki yake

7 Unaweza msaidia mtu kwa wema ukaonekana unajipendekeza

8 Ukiwa na ukaribu na boss au mtu mkubwa watakutunga majina kama CHAWA n.k

9 Ukiwa mgeni maeneo hasa makazini n.k kuna wadau watataka kukuchimba vya ndani kabsa kuhusu wew yani akujue tu kwa mapana

10 Unaweza chukiwa na mtu yeyote wakat wowote bila sababu yoyote hata kama hamjawahi kuongea zaidi ya salamu

11 Unaweza vile vile kuibiwa mchana kweupe huku watu wanaona na wasifanye chchte

12 Wanawake wengi hujiona ma celebrity hasa madem wa TikTok huku wakitaka kutumiwa hela bila kufanya kazi yyte

13 Unafiki umeota mizizi kuanzia level ya familia hadi huko mtaani

14 Ukiwa huna time na mtu wanasema unajisikia n.k

15 Watu wanaweza kukuangalia mpaka unaangamia bila ya msaada wwte ili wafurahi

16 Asilimia kubwa mtu wko wa karibu ndo huyo huyo atakayekuangamiza kama sio kukupeleka kaburini kbsa

Zingne naomba muendeleze
 
17. kuteseka hua wanaona ni kama mashindano,utamwambia mimi niliteseka na jambo fulani halafu atakwambia "hujateseka wewe,niulize mimi nilivyoteseka"

18.Akifa mtoto wa masikini wanasema Mungu kampenda zaidi,akifa mtoto wa tajiri wanasema katolewa kafara.

19.Kwenye chombo cha usafiri chenye uwezo wa kupitisha mtu mmoja mlangoni,watagombania ili waingie hata watu watatu kwa pamoja.

20.Mtu wa kawaida mtaani siku akivaa suti wanamsema eti anaringa.
 
Kwenye mijadala ya maana hawataki ila ngoja unazishe mada zinazohusu ngono na nguvu za kiume, hapo utajua kila mmoja amesomea.
 
Back
Top Bottom