Tabia ni ya kuzaliwa nayo au ya kujifunza?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kwa ngazi ya Kimataifa, Watanzania wanafahamika kuwa ni wapole, wakarimu, na wengine huwatuhumu kuwa ni waoga, na wavivu waliozubaa!

Wakenya wanafahamika kwa ubunifu na kujua kuchangamkia fursa ndani na nje ya mipaka ya nchi yao!

Wanigeria wanasifika kwa ujasiri na unanjaujanja mwingi. Ukizubaa unatapeliwa.

Tukirudi nchini kwetu, karibia kila kabila lina sifa inayolitambulisha:
1. Wakurya: ujasiri, ukorofi

2. Wachaga: wapenda biashara na kubebana kwenye fursa

3. Wakinga: wabishi, wafanyabiashara, na hasira

4. Waha: wabishi na wapenda biashara ya maduka

5. Wazaramo: wapenda Ngoma, waongeaji sana

6. Wahaya: wapenda Elimu/usomi

7. Wamasai na Wasukuma: wafugaji maarufu

Nini kilichowafanya watu wa jamii fulani kuwa na tabia inayowatofautisha na jamii zingine? Ni suala la DNA, kwamba wamezaliwa nazo?

Ni suala la kimazingira na kimalezi, kwamba wamejifunza?

Inawezekana kufanya uwekezaji kubadilisha tabia hasi za jamii fulani kwa maslahi mapana ya jamii husika na Taifa kwa ujumla?
 
Sioni kama kuna tabia ya jamii fulani ya kuzaliwa ila naona tu kuna namna watu wanaoishi pamoja hupenda kuigana na kushinda ,jambo hilo huzalisha mfanano kwa jamii husika.
Kama Taifa, tunaweza kufinyanga tabia za watoto wetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo?
 
Inawezekana ila shida inakuja pale kwenye kushindana na wenyewe ushawishi ambao walishajijenga na kuivuta Dunia upande wao na tabia zao Kwa kigezo Cha hapa Tz Kwa aslimia kubwa ni mbovu.
 
Kutangulia siyo kufika mkuu, ila kufika ndiyo muhimu.
 
Yes, kuna inherited traits na adoptive traits. Inherited traits zinahusisha vinasaba toka kwa wazazi. Adoptive traits zinakuja baada ya kuzaliwa na hutokana na mazingira anayokulia mtu tangu kuzaliwa. Watu hawazaliwi wezi au Malaya bali ni mazingira yanawafanya hivyo kwa maana kwamba wana adopt/kuiga

Lakini kuwa mpole au na hasira ni tabia ambazo mtu anazaliwa nazo huwezi kuiga
 
Asante🙏. Ni kama introvert na extrovert. Wanazaliwa na hizo sifa.
 
Kwa ngazi ya Kimataifa, Watanzania wanafahamika kuwa ni wapole, wakarimu, na wengine huwatuhumu kuwa ni waoga, na wavivu waliozubaa!

Wakenya wanafahamika kwa ubunifu na kujua kuchangamkia fursa ndani na nje ya mipaka ya nchi yao!

Wanigeria wanasifika kwa ujasiri na unanjaujanja mwingi. Ukizubaa unatapeliwa.

Tukirudi nchini kwetu, karibia kila kabila lina sifa inayolitambulisha:
1. Wakurya: ujasiri, ukorofi

2. Wachaga: wapenda biashara na kubebana kwenye fursa

3. Wakinga: wabishi, wafanyabiashara, na hasira

4. Waha: wabishi na wapenda biashara ya maduka

5. Wazaramo: wapenda Ngoma, waongeaji sana

6. Wahaya: wapenda Elimu/usomi

7. Wamasai na Wasukuma: wafugaji maarufu

Nini kilichowafanya watu wa jamii fulani kuwa na tabia inayowatofautisha na jamii zingine? Ni suala la DNA, kwamba wamezaliwa nazo?

Ni suala la kimazingira na kimalezi, kwamba wamejifunza?

Inawezekana kufanya uwekezaji kubadilisha tabia hasi za jamii fulani kwa maslahi mapana ya jamii husika na Taifa kwa ujumla?
Zipo AINA NYINGI ZA TABIA IKIWEMO YA KUZALIWA KUJIFUNZA AU KUIGA
 
Tabia hutokana na malezi au makuzi ya mtu.
Mahali unapokulia au kuishi kunachangia vikubwa sana katika tabia yako.
 
Sijui nipo deep sana, unauliza tabia, ila mbona kama ulizoandika hapo sio tabia ni tamaduni......
 
Back
Top Bottom