Tabia nilizozishuhudia kwa baadhi ya wanaume wa Dar


Eee eee basi mnakula vitu vya ajabu mkurya akajua kukaanga chips aisee ajabu mchaga kuimba taarabu
 
kwa ufupi ni kwamba mnakurupuka, kwa sababu thread zote hizi zililetwa baada ya ishu ya panya road, huo ni unafiki, kwani hapo hamkutuona? kwanini hamkusema?maisha bila unafiki hayaendi
 
Najiuliza vipi kama tukio lililotokea Amboni Tanga,kama lingetokea Dar es salaam,sijui safari hii ingekuwaje kwa wanaume wa Dar.
 
ingekuwa shida... nashukuru walioigiza walilitambua hili mapemaa
 
kuna nyimbo moja waliimba mwana fa na j mo INGEKUWA VIPI?
 
wenye pub zote mjini dar wangefunga loss mwezi mzima
 
Wazee wa miguu ya kuku washukuru ccm imefanya mipango yao mbali kidogo hata hivyo natumaini walitetemeka.cheza na mipango ya ccm.
 
na wao ndo hawaamini kuwa hii ni picha ya kuigiza
 
Habari za mchana mabibi na mabwana. Nina uhakika leo wengi mpo nyumbani au mmeenda matembezini kujinafasi na hii sikukuu ya Pasaka. Wengine pia mpo kazini mkipiga kazi.

Sio lengo langu kuongea kuhusu watu hasa wanaume, na sisi vijana wa shoka ambao ni wa "mkoani" kama tunavyoitwa na wana Dar slum SIO HULKA YETU ila kwa sababu ni wanaume wa hapa Tanzania, tunaguswa na kushangazwa na mienendo ya wanaume wa Dar slum.

Baada ya kuwepo Dar Slum kwa muda wa mwezi mmoja nikifuatilia dili langu fulani, hatimaye nilifanikiwa na kurudi mkoani.

Ila ukweli ni kwamba nimeshangazwa sana na wanaume wa Dar. Asilimia 90% wana haya yafuatayo ambayo kwa mwanaume wa kawaida rijari kama sie wa mikoani huwezi tukuta na hizi tabia;

Wanaume wa Dar Slum:

1. Wanawake wao wanalalamika hawawaridhishi kitandani,

2. Wengi wanalia lia tu kila wanapoombwa hela na wapenzi wao, eti wanataka usawa,

3. Wengine wamewekwa ndani na wanawake, yaani wanalelewa.

4. Wana vitambi, yaani unakuta kijana mdogo kabisa na ni mwembamba ila kitambi hicho,

5. Wanatinda nyusi,

6. Nao wanaoshwa kucha za miguuni na wanaume wenzao.

7. Wanalia lia hamna kazi ila wanachagua kazi za kufanya,

8. Unakuta jibaba zima liko juu ya miaka 25 ila linakaa kwa baba na mama au bado ni tegemezi,

9. Wako dhaifu sana, hawana tabia ya kufanya mazoezi ya kuimarisha afya, wakivamiwa makwao ni full kukimbia kuomba misaada kwa majirani ambao nao ni wanaume wale wale, kitu ambacho sisi wanaume wa mikoani kama kuna ishu ya mabavu na busara huwa tunaimaliza kishujaa,

10. Wanaogopa kuja MIKOANI ambako ndo kuna hela,

11. Makaka poa wapo kila kona na wanaume wengine wanaona eti ni kawaida kuwa Mungu aliwaumba hivyo,

12. Wavivu, unakuta yupo ktk basi na kuna foleni yeye anaenda sehemu ambayo ni kama mita 300 toka liliposimama basi ktk foleni ila yuko tayari asubiri hata dk 50 ndani ya basi.

13. Wanaume Wenye magari wanatembea na madumu ya mafuta,

14. Wachafu, Ukienda mahali wanapoishi kwa wale walio mabachelor ni kama zizi la ng'ombe,

15. Wanaume wanakojoa kojoa popote tu barabarani kama mbwa,

16. Kwa wale vijana unakuta kavaa suruali kaweka chini ya makalio na anaona ni sawa tu kuonyesha nje nje nguo yake ya ndani tena chafu,

17. Unakuta wanaume wenye familia jioni wamekaa kwenye kahawa na kashata wanaongea umbea,

18. Etc

Kwa kweli nimeshangazwa sana na hawa wanaume wa Dar, hayo ni baadhi ya mapungufu yao, ila yako mengi sana!

Na jiji lenyewe ni KERO. Isiponyesha mvua ni jua kali, joto foleni na vibaka, ikinyesha mvua ni matope, madimbwi ya maji hadi mjini posta.

Kwa kifupi, wanaume wa Dar Slum mjirekebishe, wanaume hatitakiwi kuwa hivyo! Mtuige sisi wa mkoani.
 
Uliyoyaorodhesha ni mambo ambayo yapo na yanapaswa kweli kupiga vita
cha ajabu wanao toka mikoani wakija Dar baada ya wiki chache ndo wanakuwa
mara mbili au tatu zaidi

mtu kwao anatembea kilomita 20 kila siku kwenda kulima
lakini posta na kkoo anataka Bajaj.......

ingekuwa wa mikoani mkija mnaonesha tofauti na wa Dar pia wanngejiuliza

asilimia 80 ya wakazi wa Dar hawajazaliwa Dar....wametoka huko huko mikoa tofauti...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…