Tabia ya kuchanganya content kwenye social media account za kibiashara, inatukosesha Sana wateja na Kama sio wote Basi wateja serious tunawapoteza

Little Dreamer

Senior Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
180
Reaction score
162
Habari wadau, nikiwa Kama kijana naepambana katika kizazi hiki Cha teknolojia, Mimi ni mdau mkubwa Sana wa mitandao ya kijamii, na ni miongoni mwa watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii kujipatia kipato.

Moja ya vitu nilivyo vi observe na nikaona vinatugharimu Sana hasa kwenye mtandao wa Instagram na Facebook ni tabia ya kupost kwenye account za kibiashara post ambazo hazihusiani na biashara husika. Yaani mfano, mtu anadeal na ujenzi au uchoraji ramani lakini humo ndani kapost memes ambazo hata hazihusiani na kazi ya ujenzi.

Au mtu anahusika na uuzaji wa magari lakini humo ndani anapost kuhusu topics za mahusiano na jokes mbalimbali ambazo "they have nothing to do with the business" Au mtu anauza nguo lakini humo Tena anatoa ushauri kuhusu mapenzi, Mara anapost videos za ajali n.k

Hakuna shida na memes Wala Mada nyingine za mitandaoni, Ila wateja au wafuasi wa mitandao wanafatilia post husika kwa kuvutiwa na huduma zinazoonekana kwa account, kupost both visivyohusiana kutawafanya baadhi ya wateja kukereka kwa nanna moja ama nyingine na inaweza kuwa changamoto ya biashara kufanikiwa.

Ushauri wangu kwa wafanyabiashara wanaotumia mitandao, ni bora kubakia kwenye lengo kuu la akaunti zetu, na Kama lengo ni kuvutia wateja kupitia ucheshi n.k, ni bora kutumia ubunifu kwa kutengemeza content inayohusiana na biashara yako na kuweka ucheshi ndani yake, Kama huna uwezo huo Basi sio vibaya kujifunza, hivo ndivyo tunavyokua.

Naomba kuwasilisha!
 
Mkuu hio market strategy saivi ukisema unakomaa na kupost biashara peke yake napo kuna time watu wanakuchoka sasa wanafanya kutafuta namna yakufatiliwa kwa wingi at the end of the day wateja watakuja tu wew angalia kama room of jeans utajua watu wanachofanya... saivi biashara ni sanaa na ubunifu
 
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana na hili lipo sana, unakuta mtu anafanya biashara ya nguo, status 4 za mwanzo ni nguo, ya 5 na ya 6 ni memes, ya 7 ni nguo. Tayari hapo mtu anaona kuna ubabaishaji.
Sidhan kama ni ubabaishaji bali nahs ni marketing strategy mfano sasa hv kuna ile wengi wanatumia kuunganisha video ya kuchekesha na biashara mwishon mfano mtu anakimbizwa na mbwa had anadondoka then mtu anaeuza nguo anajifanya yy ndo kadondoka na hapohapo anaanza ku market nguo zake [emoji23][emoji23] its fun maana inamfanya mteja awe kwenye suspense kumaliza video nzima.
 
Bora iwe hivyo kuna watu hizo video hazihusiani kabisa na tangazo la kibiashara.
 
Mkuu umetoa ushauri mzuri sana na hili lipo sana, unakuta mtu anafanya biashara ya nguo, status 4 za mwanzo ni nguo, ya 5 na ya 6 ni memes, ya 7 ni nguo. Tayari hapo mtu anaona kuna ubabaishaji.
Kuna jamaa akaunti yake ni ufugaji wa samaki kibiashara, lkn humo kaweka picha zake kibao akiwa ameachilia bonge la tabasamu.

Kuna baadhi ya akaunti makini ,wanaweka baadhi ya post ili ku interact na followers wao ( Hii ni mbinu).
 
Sasa anaweka picha zake ye ni samaki? Anakosea
 
Ni nzuri kuvuta mteja kukupa attention ila iwe kwa kiasi
 
Kuna jamaa mmoja ana duka la nguo, utakuta ameweka status WhatsApp picha ya kwanza tangazo la biashara yake, status ya pili kaweka memes, status ya 3 kaweka picha yake akiwa maeneo yakujidai.

Kesho yake ukiangalia status yake utakuta kaweka status ya mwamposa, na ma status ya neno la mungu kibao. Sasa huwa najiuliza huyu mtu katika biashara anayoifanya yupo serious kweli?

Je anajua umuhimu wa hii mitandao katika biashara yake?
 
...
 
Habari wadau, nikiwa Kama kijana naepambana katika kizazi hiki Cha teknolojia, Mimi ni mdau mkubwa Sana wa mitandao ya kijamii, na ni miongoni mwa watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii kujipatia kipato.

Moja ya vitu nilivyo vi observe na nikaona vinatugharimu Sana hasa kwenye mtandao wa Instagram na Facebook ni tabia ya kupost kwenye account za kibiashara post ambazo hazihusiani na biashara husika. Yaani mfano, mtu anadeal na ujenzi au uchoraji ramani lakini humo ndani kapost memes ambazo hata hazihusiani na kazi ya ujenzi.

Au mtu anahusika na uuzaji wa magari lakini humo ndani anapost kuhusu topics za mahusiano na jokes mbalimbali ambazo "they have nothing to do with the business" Au mtu anauza nguo lakini humo Tena anatoa ushauri kuhusu mapenzi, Mara anapost videos za ajali n.k

Hakuna shida na memes Wala Mada nyingine za mitandaoni, Ila wateja au wafuasi wa mitandao wanafatilia post husika kwa kuvutiwa na huduma zinazoonekana kwa account, kupost both visivyohusiana kutawafanya baadhi ya wateja kukereka kwa nanna moja ama nyingine na inaweza kuwa changamoto ya biashara kufanikiwa.

Ushauri wangu kwa wafanyabiashara wanaotumia mitandao, ni bora kubakia kwenye lengo kuu la akaunti zetu, na Kama lengo ni kuvutia wateja kupitia ucheshi n.k, ni bora kutumia ubunifu kwa kutengemeza content inayohusiana na biashara yako na kuweka ucheshi ndani yake, Kama huna uwezo huo Basi sio vibaya kujifunza, hivo ndivyo tunavyokua.

Naomba kuwasilisha!
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom