ok mtoa mada kama umoa basi nadhani sio mda mrefu
ndoa ina mambo mengi na visa vingi vilivofichwa ktk pazia la chumbani
kama umebarikiwa ndoa yako iko sawa na mnaishi kadiri ya mapenzi yenu nawapa hongera
wapo wanaotoka nje ya ndoa kwa kutoridhishwa na wenzi wao,wengine tamaa,wengine maudhi
wengine washazoea tangu mwanzo kutokuwa na mpenzi mmoja
wengine wanatafuta ladha tofuati nk,una haki kuwashangaa lakini usijihesabu utakuwa mkamilifu daima labda kwa uweza wa Mungu pekee, nimekumbuka kisa kimoja jamaa yetu mmoja alikuwa akikosoa kila mara watu wanaosaliti ndoa zao
siku moja alichelewa kufika home kwake alipitia small house
kujiongezea nguvu kumbe baada ya shughuli akajisahau alishtuka saa 8 usiku huku simu yake ina missed calls kama 20 hivi za mkewe
asbh alidamkia oysterbay akaongea na polisi mmoja wa zamu akampa sh 50,000 akamwomba ampigie mkewe simu kumjulisha yupo kituoni eti kakamatwa usiku akiendesha gari akiwa amelewa akaambiwa amdhamini kwa sh 50,000
mke kwa pendo lake alikuja haraka kumdhamini mumewe asijue kafanyiwa usanii na mumewe
hadi leo mkewe hajui labda kisoma hii habari lkn yashapita.
.