Tabia ya kujipapasa usoni kila mara ni ugonjwa gani huu?

Sunshow

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
1,140
Reaction score
395
Kuna jamaa mmoja kila mara hujipiga piga usoni na kujipapasa kana kwamba kuna wadudu wanamshambulia. Haiwezi kupita sekunde ishirini bila kurudia kitendo hicho. Najiuliza huu ni ugonjwa gani na tiba yake ni ipi?

Mkiwa kwenye maongezi anakuwa kero.

Watu wake wa karibu wanasema hii tabia amekuwa nayo toka kitambo.
 
Wataalamu wa magonjwa ya binadamu njooni anga hizi.
 
Bora huyo kuliko wale wanaoingiza vidole puani kila baada ya dk kadhaa
 
Nadhani ni tabia tu iliyosababishwa na mazowea,kwanini msimuulize muhusika mwenyewe kua hua anahisi nini hasa mpaka kujipapata uso kila mara? Huenda ukapata jibu sahihi toka kwake kuliko humu.
 
Papasitis?
On a serious note, pengine ni tabia tu aliyojijengea bila sababu maalum, au ana:-
1,Anxiety disorder (wasiwasi).
2, Tourette Syndrome- kupepesa macho mara kwa mara, kukohoa hoa mara kwa mara kama vile kuna kitu kimenasa kooni, kunusa nusa hovyo hovyo, kuongea bila kukusudia mara kwa mara ni lugha chafu (coprolalia), mienendo ya mikono/mabega ambayo hayana sababu maalum (motor tics). NK.
3, Obsessive Compulsive Disorder (OCD): Kwenye compulsion kuna kitu kinaitwa "repeatitive ritualistic activities" yaani ni vitu mtu anafanya mara kwa mara ambavyo havina maana yeyote kwa mtu mwingine, anaweza kugusu paji la uso mara tatu kufuatia na kusafisha koo na kuguna mara mbili. Hii inamsaidia kupunguza wasiwasi.

Kama hiyo tabia haimdhuru yeye binafis au watu wengine basi hakuna shida hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…