KERO Tabia ya kujisaidia haja ndogo pembezoni mwa Daladala Stendi ya Daladala Mbezi Luis inakera sana

KERO Tabia ya kujisaidia haja ndogo pembezoni mwa Daladala Stendi ya Daladala Mbezi Luis inakera sana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna tabia ambayo hasa inafanywa na Madereva na Makondakta wa Dalalda kujisaidia haja ndogo pembezoni mwa magari yao wakati yakiwa kwenye foleni hasa magari yaendayo shamba yaani Mlandizi, Boko Mnemela, Chalinze na Miono inaendelea kukithiri.

Taboa hiyo imesababisha kuwe na harufu mbaya sana kwa Watumiaji wa Miundombinu ya kituo hicho, pia inahatarisha afya na kupelekea mlipuko wa magonjwa.

Kuna Watu wanafanya biashara ya Vyakula na vitafunwa, sasa hicho kinachoendelea kinaumiza wengi na kinaweza kuwa na athari kubwa kibiashara na kiafya.

Mamlaka za usimamizi wa kituo hichi zipo wapi?
 
Back
Top Bottom