Tabia ya kuogopa ukweli unaoumiza inaweza kukukwamisha njiani

Tabia ya kuogopa ukweli unaoumiza inaweza kukukwamisha njiani

Mwangazza

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
34,153
Reaction score
51,777
Wengi wetu hatupendi ukweli unaotusumbua. Tunapenda kinachotufanya tuonekane tuko sahihi hata kama tunajua tumekosea. Hatupendi kuwajibika. Tunapenda wapambe wanaolinda makosa yetu. Hatupendi kujifunza. Tunapenda kuendeleza kile kile tulichowahi kukijua. Hatupendi kubadilika. Tunapenda kulinda ‘heshima’ hata kama tunajua hatujiheshimu.

Nilikuja kusoma kuhusu uwiano kati ya hisia na mantiki.
Tunatumia miaka 20+ kujifunza jinsi ya kutumia mantiki, ila tuna elimu kidogo sana kuhusu hisia.
Hivyo basi chochote kinachoamsha hisia ngumu,tunakichukia,na kukimbia, tunasaka vinavyoamsha hisia tamu.
Emotions Vs Logic
 
Back
Top Bottom