Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Nchi ya UAE inayounganisha na jimbo la Dubai ni miongoni mwa mataifa tajiri sana duniani.Kila kitu wamependelea kiende kiteknolojia hata pasipokuwa na umuhimu wa namna hiyo.
Maendeleo hayo ndiyo yamewafanya wasiweze kusubiri mvua zinyeshe kwa hiyari yake japo hawana shida sana ya maji wala upungufu wa chakula.
Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990 nchi hiyo ndipo ilipoanza tabia ya kuvuna mawingu ambayo yamekaribia kutunga mvua.
Ndege zenye madawa hurushwa angani na kwenda kuyarushia makombora yenye dawa mawingu hayo ambapo haraka huunda mvua na kunyesha eneo wanalotaka.
Mfumo huo wa kuvuna mawingu umewahi kutumika sana kwenye nchi ambazo hazimjui Mungu vyema kama vile Marekani na kwengineko.
Taarifa za wafuatiliaji wa nyenendo za ndege wamesema waliziona ndege mbili za kazi hiyo zikiruka siku za Jumatatu na Jumanne kuelekea kwenye mawingu ikiwa ni siku moja tu kabla ya mafuriko ya ghafla yaliyoikumba nchi hiyo.
Wahusika wa idara ya hali ya hewa walipofuatwa kuulizwa kuhusu zoezi hilo walikataa kuzungumza na waandishi wa habari.
Mafuriko hayo yamepelekea barabara kuu za jjji la Dubai na miji jirani kufungwa baada ya kugeuka kama mito.Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai kwa upande wake uligeuka kama ziwa kubwa kama maziwa ya nchi za kiafrika.
Misafara ya ndege kwenye uwanja huo imesitishwa kwa muda na kupelekea zahma ambayo haijawahi kutokea .Tayari watu kadhaa wameripotiwa kufariki katika nchi hiyo na nchi jirani ya Oman.