Tabia ya kuwapandisha kwenye daladala watu wanaoomba msaada sio nzuri

Ricky Blair

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
463
Reaction score
1,009
Hii tabia ya kuwapandisha omba omba ambao ni watu sio kwamba nawachukia au kuwahukumu ingawa maisha yao duni yanachukiza kwa yoyote anayechukia umaskini; Ila tabia ya kuwapandisha daladala au kuwaingiza sehemu kwa ajili ya kuomba hela sio sawa wengine vipofu.

Watu wasipomsaidia je? Na pia watu hata Km hela tunazo hatuwezi kutoa kila saa au kila siku coz TZ 80% masikini wa kufa ingawa wengi hawaombi Ombi Bali wanahangaika na kazi duni. Hawa vilema ambao wanaomba omba wapewe sehemu yao rasmi ya kuwapa Msaada Km vituo vya watoto yatima.

Sio barabarani au kuingia kw mabasi au barabarani ambao ni hatari sana sana kwa vilema ya macho au viungo. Pia wengine wanakuja kwa nembo ya kuhubiri Yesu au Allah Kisha kuomba hela( Cjui why uyo Mungu hasaidii kitu) Jaman umaskini unachefua nataman wote tupotee tu.

Cjui hao wanaoweza kuamini Mungu wanamchukuliaje uyu Jamaa yupo kimya tu na majanga kila kona.
 
Kuna wale unakuta mwaka mzima anachangisha hela ya kwenda hospitali...yaani unaweza shangaa baada ya miaka miwili tena bado anasema anatakiwa kwenda hospitali...
 
Sio barabarani au kuingia kw mabasi au barabarani ambao ni hatari sana sana kwa vilema ya macho au viungo. Pia wengine wanakuja kwa nembo ya kuhubiri Yesu au Allah Kisha kuomba hela( Cjui why uyo Mungu hasaidii kitu) Jaman umaskini unachefua nataman wote tupotee tu. Cjui hao wanaoweza kuamini Mungu wanamchukuliaje uyu Jamaa yupo kimya tu na majanga kila kona.
Usisahau wengine baada ya kuomba mchana kutwa jioni unamkuta amebambia demu kilabuni eneo la starehe wanakula vitu.

Baada ya kujuwa hili suala la kuwasaidia binafsi nilipunguza kabisa.

Wengine matapel wengine wezi shida tupu.

2019
Kuna jamaa alikuja eneo la kazi ALBINO mtu mzima mkono kafunga bandeji kwa maelezo kuwa kakatwa kiganja.

Pia akadai mtoto wake yuko hospital kakatwa mkono, Story ikatugusa tukamchangia kazini, aliyetoa elfu 10, elfu 5, buku, buku 3 akapata kweli pesa.

Jioni tukamkuta eneo anapiga vitu bandeji kafungua kumbe mzima wa afya kabisa.
 
Au ile siku umeamua kujibless umeagiza kakihepe chako, tumishkaki tuwili na kapepsi mara hao wanatia timu wanakukazia ukijiangalia umebaki na kama jero tu la nauli, yaani unakula huku unajishtukia.
 
Kuna wale unakuta mwaka mzima anachangisha hela ya kwenda hospitali...yaani unaweza shangaa baada ya miaka miwili tena bado anasema anatakiwa kwenda hospitali...
Kuna wale wa barabarani yupo kwenye wheelchair halafu anaye msukuma ni kidume chenye nguvu zake.

Sasa hapo ukisaidia unasaidia watu wa ngapi? Kwanini huyo mwenye nguvu anae msukuma asinde kufanya kazi ili amtunze huyo mlemavu?
 
Usisahau wengine baada ya kuomba mchana kutwa jioni unamkuta amebambia demu kilabuni eneo la starehe wanakula vitu.

Baada ya kujuwa hili suala la kuwasaidia binafsi nilipunguza kabisa.

Wengine matapel wengine wezi shida tupu.

2019
Kuna jamaa alikuja eneo la kazi ALBINO mtu mzima mkono kafunga bandeji kwa maelezo kuwa kakatwa kiganja.

Pia akadai mtoto wake yuko hospital kakatwa mkono, Story ikatugusa tukamchangia kazini, aliyetoa elfu 10, elfu 5, buku, buku 3 akapata kweli pesa.

Jioni tukamkuta eneo anapiga vitu bandeji kafungua kumbe mzima wa afya kabisa.
Hukudai pesa yakoo?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Au uli mfananishaa??
 
Mimi nasema hawa wasiojiweza na wenye changamoto za ulemavu ukiwasaidia ujue ndio ibada yenyewe hiyo na utapata thawabu. Mimi kilio changu ni ongezeko la wahubiri ambao wanalitumia neno kwaajili yao na sio kwa lengo la Mungu. Ni mahubiri yasiyowataka tena watu waache dhambi, ni mahubiri yasiyozungumzia tena habari za Maisha mapya ya Mbinguni kama ilivyokuwa 1970 - 1990. Sasahivi ni mahubiri yakucheza na changamoto za mwilini na kuwapa watu matumaini ya shida zao na mafanikio, LENGO NIKUWALEGEZA ILI WATOE HELA. SASAHIVI NI VURUGU KILA SEHEMU .

Watumishi wa kweli walikomea mwaka 1990, baada ya hapo ni wamekuja matapeli. Chakusikitisha zaidi hadi kanisa la kkkt lililokuwa na Misingi mizuri katika imani nalo limeshabadilika sana na ukiingia ibadani neno la Mungu sio kipaumbele tena bali Maisha ya mwili na Michango, matamasha, biashara nk na ndio mwanzo wa KUIBUKA KWA VIBURI KWA BAADHI YA WATUMISHI KAMA YULE WA K/NYAMA NA KIMARA na Kanisa kuonekana ni dogo kuliko Mtumishi. Pia wengi wa wahubiri wanaojiita walokole wametokea kkkt.

Makanisa angalau bado yamesimama kama taaasisi imara katika Imani na kuheshimu utaratibu ni KANISA KATOLIKI NA KANISA LA KISABATO
 
Msaada waniombe mm jinsi ya kuwasaidia unipangie ww.Kweli Dunia Duara
 
Wengi wao matapeli, wamewaharibia wenye shida genuinely.
 
famlia zetu zina walemavu na wanajituma na hawawezi kuhesabika ni watu wa kusaidiwa....huwa nawachana makavu kama karma iwe..maana hata babangu ni mlemavu na sijawahi ona akiomba au akipokea msaada zaidi ya kusaidia.
 
Hii tabia ya kuwapandisha omba omba ambao ni watu sio kwamba nawachukia au kuwahukumu ingawa maisha yao duni yanachukiza kwa yoyote anayechukia umaskini; Ila tabia ya kuwapandisha daladala au kuwaingiza sehemu kwa ajili ya kuomba hela sio sawa wengine vipofu.

Watu wasipomsaidia je? Na pia watu hata Km hela tunazo hatuwezi kutoa kila saa au kila siku coz TZ 80% masikini wa kufa ingawa wengi hawaombi Ombi Bali wanahangaika na kazi duni. Hawa vilema ambao wanaomba omba wapewe sehemu yao rasmi ya kuwapa Msaada Km vituo vya watoto yatima.

Sio barabarani au kuingia kw mabasi au barabarani ambao ni hatari sana sana kwa vilema ya macho au viungo. Pia wengine wanakuja kwa nembo ya kuhubiri Yesu au Allah Kisha kuomba hela( Cjui why uyo Mungu hasaidii kitu) Jaman umaskini unachefua nataman wote tupotee tu.

Cjui hao wanaoweza kuamini Mungu wanamchukuliaje uyu Jamaa yupo kimya tu na majanga kila kona.
Mkuu hawapandishwi na dreva wala konda hupanda kama abiria na wengine hulipa kabisa nauli, sasa konda ataanzia wapi kumshusha ikiwa nauli yake kalipwa, kwa hiyo hawezi kurudisha hela kisa ombaomba.
 
Kuna wale wa barabarani yupo kwenye wheelchair halafu anaye msukuma ni kidume chenye nguvu zake.

Sasa hapo ukisaidia unasaidia watu wa ngapi? Kwanini huyo mwenye nguvu anae msukuma asinde kufanya kazi ili amtunze huyo mlemavu?
Hawa wa barabarani mimi watanisamehe.

Mwaka flani hivi iliwahi kujulikana nyumba flani ziko Manzese, nyumba ambazo zinafuga hao walemavu.

Ni mradi wa mtu ameamua kuwakusanya walemavu na kuwaweka humo kila asubuhi wanaenda mtaani kuomba then jion wanaleta hesabu kwa boss.
Wao wanalipwa kula tu.
Na kilichoniumiza ni jinsi wanavyoishi pale na treatment.. Siyo fair kabsa.

Yule waziri aliamua kuwaadhibu kwa bakora wamiliki wa biashara na nyumba zile.
 
Hii tabia ya kuwapandisha omba omba ambao ni watu sio kwamba nawachukia au kuwahukumu ingawa maisha yao duni yanachukiza kwa yoyote anayechukia umaskini; Ila tabia ya kuwapandisha daladala au kuwaingiza sehemu kwa ajili ya kuomba hela sio sawa wengine vipofu.

Watu wasipomsaidia je? Na pia watu hata Km hela tunazo hatuwezi kutoa kila saa au kila siku coz TZ 80% masikini wa kufa ingawa wengi hawaombi Ombi Bali wanahangaika na kazi duni. Hawa vilema ambao wanaomba omba wapewe sehemu yao rasmi ya kuwapa Msaada Km vituo vya watoto yatima.

Sio barabarani au kuingia kw mabasi au barabarani ambao ni hatari sana sana kwa vilema ya macho au viungo. Pia wengine wanakuja kwa nembo ya kuhubiri Yesu au Allah Kisha kuomba hela( Cjui why uyo Mungu hasaidii kitu) Jaman umaskini unachefua nataman wote tupotee tu.

Cjui hao wanaoweza kuamini Mungu wanamchukuliaje uyu Jamaa yupo kimya tu na majanga kila kona.
Huyu Mungu badala atimize wajibu wake anasubiri mpaka watu wamuombe.
 
Back
Top Bottom