Tabia ya kuweka akiba kila unapopata pesa ni mbaya sana

Tabia ya kuweka akiba kila unapopata pesa ni mbaya sana

mr pipa

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
4,335
Reaction score
9,286
Umepata ka laki mbili, au kaelfu hamsin unakaweka akiba utazani ndio mwisho wa utafutaji na haupati tena.

Hizo ni dalili za umaskini na wewe ni mvivu wa utafutaji hela.

Ukipata hela irudishe yote kwenye mzungu sio mnazihifadhi kama wale mafisani wanaoenda, kuweka pesa mabenki ya nje matokeo yake, mzunguko unakuwa mdogo, hela inakuwa haionekani mtaani.

Wewe nunua kitu ndio ukiweke akiba, kama kuku anafaa nunua waweke, kama kiwanja, vyovyote.

Tukisema kila mmoja hapa nchini aweke akiba pesa yake anayopata, kusingekuwa na pesa mtaani, na serikali ingekuwa inachapisha pesa kila kukicha.

Acha tabia mbaya ya kujifanya unaithamini pesa kwa kuitunza unatusababishia mzunguko kuwa mgumu.

HONGERENI NYINYI MNAOPATA PESA MNAHAKIKISHA MNAIMALIZA YOTE NYIE NDIO MNAJUA KUTAFUTA PESA
 
Nadhani akiba ni ile pesa inayobaki baada ya kufanya mambo yote ya msingi, ndo mana ukiangalia bajeti nyingi ishu ya akiba hua ipo mwishoni kabisa.
 
Ishu wala sio kuweka akiba.weka katik mifumo rasmi
Hiv unafikr ile mil 1 yako benk imekaa tu? Ipo kwenye mzunguko.
 
Back
Top Bottom