Tabia ya 'ma-star' kulazimisha umaarufu kwa watoto wao ni hatari

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
Hata kama unapenda kula pilau huwezi kuvua samaki kwa kuweka pilau kwenye ndoano. Hata siku moja usifikiri kwa vile wewe unapenda kitu flani basi watoto, ndugu na rafiki watakipenda.

Sio vibaya kwa mastaa kuwawish watoto wao birthday au kupiga nao picha chache lakini kumezuka hali ya mastaa kuwafanya watoto wao kuwa celebrities kwa kuwafungulia account instagram zikiwa na followera wengi ambao hata maskini ya Mungu huyo mtoto hajapata hata akili ya kujua watu. Isitoshe kuna wengine washafanya watoto wao waingie mikataba na makampuni kwa kutumia picha za mtoto kwa biashara. Huku ni kulazimisha ustaa kwa watoto wao kitu ambacho wanaweza kuja kujutia au mtoto anaweza kuja kujutia.

Hivi ushawahi kufikiri kumpa ustaa mtoto wako ikatokea anaanza shule na kwa bahati mbaya akawa mbumbumbu kupita kiasi na mbaya zaidi kila kona ya mtaa tanzania nzima akiitwa majina asiyoyapenda sababu kuu ikiwa wazazi wake?

Ije itokee mtoto ana soma comments na anakutana na haters wanatukana yeye na wazazi wake, hivi huyo mtoto si atapata stress mapema. Kwa ufupi kuwaamulia hawa watoto maisha yao yawaje ni vibaya kwa kiasi lakini kwa huu mwendo wa kumfanya mtoto awe star huku hajui ni nini kinaendelea inaweza ikaja kuwa kinyume kabisa na alivyotaka maisha yake akikua na akili maana sio kila mti hupenda umaarufu.

Kuna wazazi mastaa kwa ushamba hawajali privacy za family wanaona ni kick kumfanya mtoto awe dili lakini kiukweli mtoto anaweza kuja kuathirika vibaya sana.

Ni hayo tu!
 
Hata wasiwape kicks hao watoto watafukunyuliwa hata uvunguni chezea wabongo na ma gazeti ya udaku, walitafuta hadi mtoto wa Jk aliyekuwa anasoma muhimbili, sasa akili ya mtoto mwenyewe na ulivyomlea, we cheki sepenga umaarufu unavyomtesa mara umeme, mimba hazishiki, mara hichi kile mateso yataendelea hadi kwa vizazi vyake hasipokuwa makini
 
Siku zote ukishakuwa public figure kila kilocho kuzunguka lazima watu wakijue na wata kisema tu, watu wana ponda hata mbwa za mastaa sembuse watoto!!.
Obama pamoja na kuwa na familia nzuri ila alikuwa ana chafuliwa hadi basi, watoto wa Trump sku hizi kwenye page zao wanatukanwa vizuri tuu. Kumbukeni kina Ridhiwani, ila jamaa walikuwa hawapanic maisha yana songa tu.
Muhimu ni wazazi wao kuwafundisha kuwa watulivu na kukabiliana na shida ndio ustaa huo. Lakini pia wasiwafungie wawape exposure wakisha jijua ni wao kina nani mengine wata vumilia.
 
mastaa tunaozungumzia hapa ni watu amabao wapo kwenye fani za kucheza michezo, kuigiza, kuomba, etc
 
hao uliowataja sidhani kama walianzishiwa account instagram, na hata sidhani kama walikuwa publicized wakiwa hata hawajafika mwaka 1
Hawakuzaliwa kipindi cha instagram, mtu kama Donald angewaanzishia tuu
Wala sioni ubaya kwa mtoto anaye zaliwa zama hizi kuanzishiwa, ilimradi akikua asilazimishwe kutumia tu.
Mambo ya matusi yana vumilika
 
Hawakuzaliwa kipindi cha instagram, mtu kama Donald angewaanzishia tuu
Wala sioni ubaya kwa mtoto anaye zaliwa zama hizi kuanzishiwa, ilimradi akikua asilazimishwe kutumia tu.
Mambo ya matusi yana vumilika
Haya
 
Sahivi msanii akiwa na mimba tu, anafungua account ya kijacho, kijacho anaanza kutupa updates akiwa bado tumboni.... Kazi kweli kweli
Hahahaaaaaa.
Ila siyo kitu kizuri sana kwa mtoto,
Inaweza kuonekana ni uzungu lakini majuto huwa ni makubwa zaidi huko mbeleni.
 
Sasa wewe unamuongelea Tiffa au cook
 
Hao mastaa uchwara wenu tatizo hawana family base. Wengi wamelelewa kimamama kwahiyo alichosema mleta mada hawakijui. Kubwa zaidi Upstair wako empty. Angalia wasanii wanaojitambua kina AY, FA nk nk hawawez kuwa na mambo ya kipimbi kama hao vilaza wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…