Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,370
Hata kama unapenda kula pilau huwezi kuvua samaki kwa kuweka pilau kwenye ndoano. Hata siku moja usifikiri kwa vile wewe unapenda kitu flani basi watoto, ndugu na rafiki watakipenda.
Sio vibaya kwa mastaa kuwawish watoto wao birthday au kupiga nao picha chache lakini kumezuka hali ya mastaa kuwafanya watoto wao kuwa celebrities kwa kuwafungulia account instagram zikiwa na followera wengi ambao hata maskini ya Mungu huyo mtoto hajapata hata akili ya kujua watu. Isitoshe kuna wengine washafanya watoto wao waingie mikataba na makampuni kwa kutumia picha za mtoto kwa biashara. Huku ni kulazimisha ustaa kwa watoto wao kitu ambacho wanaweza kuja kujutia au mtoto anaweza kuja kujutia.
Hivi ushawahi kufikiri kumpa ustaa mtoto wako ikatokea anaanza shule na kwa bahati mbaya akawa mbumbumbu kupita kiasi na mbaya zaidi kila kona ya mtaa tanzania nzima akiitwa majina asiyoyapenda sababu kuu ikiwa wazazi wake?
Ije itokee mtoto ana soma comments na anakutana na haters wanatukana yeye na wazazi wake, hivi huyo mtoto si atapata stress mapema. Kwa ufupi kuwaamulia hawa watoto maisha yao yawaje ni vibaya kwa kiasi lakini kwa huu mwendo wa kumfanya mtoto awe star huku hajui ni nini kinaendelea inaweza ikaja kuwa kinyume kabisa na alivyotaka maisha yake akikua na akili maana sio kila mti hupenda umaarufu.
Kuna wazazi mastaa kwa ushamba hawajali privacy za family wanaona ni kick kumfanya mtoto awe dili lakini kiukweli mtoto anaweza kuja kuathirika vibaya sana.
Ni hayo tu!