BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Nina malalamiko kuhusu magari ya Mwendokasi, nina mambo mawili, la kwanza ni kuhusu kutotajwa kwa majina ya vituo, tabia hii ilianza mdogomdogo na hatimaye imekuwa kawaida.
Ni kama vile wanaamini kila anayepanda Mwendokasi basi anajua vituo na anaijua Dar vizuri.
Katika vituo vya hatikati ya Mji japo hawataji lakini mtu unaweza kuchungulia kituo ambacho gari inaelekea ukasoma na ukatambua umefika wapi.
Changamoto ni kutoka Kimara Mwisho kwenda Mbezi, Mloganzila na Kibaha, hapo kati hakuna anayetaja kituo, inabidi ujiongeze mwenyewe kwa kuuliza watu au kama unapajua basi uchungulie nje.
Kama makonda kwenye daladala za kawaida wanataja majina ya vituo kila siku, inakuwaje Mwendokasi inashindikana? AU ndio ile kuchukuliana poa kwa kuwa wanajua lazima watu watapanda tu huo usafiri? Nimeshuhudia watu kibao wakipitiliza vituo na kulazimima ufanya mchakato wa kurudi walipotakiwa kushuka.
Jambo la pili
Juzi nilimepata changamoto wakati nataka kusafiri, nilikata tiketi ya online kutokea Kituo cha Kimara Stop Over kuelekea Kibaha.
Nikashushwa kwenye gari na madreva wawili kwa madai kuwa hawaamini kama tiketi imekuwa scanned lakini pia kuna mmoja akasema kabisa kwamba hakuna scanner katika vitu vya katikati na hawawezi kunipakia kwa sababu nitasafiri bure.
Yaani nimebaki nimeshangaa, kwanza magari ni machache ya kwedna Kibaha ila hao madereva ndio walinichosha kabisa ikabidi nibadilishe usafiri ili niwahi kibaruni.
Kama vituo vingine vinasumbua ni bora wakasema kabisa kwamba tusilipie online.