KERO Tabia ya Shule kuchangisha pesa za mitihani kila wiki inakithiri, Walimu wameifanya kuwa mtaji

KERO Tabia ya Shule kuchangisha pesa za mitihani kila wiki inakithiri, Walimu wameifanya kuwa mtaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Shule nyingi za Msingi na hata Sekondari zimejitengenezea utaratibu wa kuwafanyisha mitihani wanafunzi hasa walio katika mwaka wa mitihani ya Taifa kama Darasa la Nne, Saba, kidato cha pili na nne. Shule hizi hulazimisha wanafunzi kuchangia mitihani hiyo ambayo huifanya kila Jumamosi. Wanafunzi wasiochangia mitihani hiyo huadhibiwa au kujengewa uadui mkubwa na walimu

Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kigamboni ni moja ya shule zenye hii tabia ya wanafunzi kuchangishwa pesa za mitihani. Yaani wao kila wiki ni mitihani, halafu Walimu hawasahihishi mitihani ila inasahihishwa na hao hao wanafunzi wanaofanya mitihani. Walimu wao wanaangalia pesa tu.

Mzazi unalipa pesa ya mitihani lakini cha kushangaza mitihani ikiletwa ukikagua unakuta mtoto kakosa ila kawekewa tiki, ukimuuliza anakuambia wanaosahisha ni wanafunzi wenzetu.

Naombeni na hili mlifikishe mtandaoni na mamlaka husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
Elimu ni Bure 100% ni kitu hakiwezekani, hii sector iko underfunded, kama mzazI unaakili, unatakiwa uwaonee huruma waalimu, siyo kuwaita ni wezi!!
 
Back
Top Bottom