Tabia ya Watanzania kupenda michango

Tabia ya Watanzania kupenda michango

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,093
Reaction score
1,899
Habari wadau,

Leo nimepata muda kujiuliza hivi hii tabia ya Watanzania (walio wengi) au jamii yetu kupenda sana tabia ya kuanzisha michango na kuchangia tumeipata wapi? Au ni ile toka enzi za siasa za ujamaa na kujitegemea?

Sipingi kuchangia mambo muhimu, ni jambo jema sana kuchangia mambo muhimu ya maendeleo.

Lakini hivi sasa tabia hii imezidi kwa kweli. Najua kuchangia si lazima ni hiari Lakini imekuwa too much!

Kila group la whatsup likianzishwa, wiki ya kwanza ya pili mchango. Wanasiasa kitu kidogo, wananchi tunaomba mchangie kidogo. Tabia hii mpka serikali kupitia viongozi wake, wanahamasisha michango, huku wakizitafuna kodi bila kujali.

Leo mtu anafungua kesi mahakamani ambayo haina gharama zozote zaidi anahamasisha umma umchangie.

Nina magroup ya whatsup takribani Matano baada ya kuyapunguza sana, lakini bado nikimaliza mchango huu, group lile linaleta michango miwili au zaidi. Matatizo ni yale yale.

Tupunguze haya mambo jamani.
 
Hii ni legacy ya Nyerere na sera zake za ujamaa

If we could go back in time ningetamani Kambona afanikiwe kupindua serikali ya Nyerere na kuintroduce capitalism from the 60s. Hii mentality ya kuombaonba hovyo kila ukiwa na shida isingekwepo.

Kila mtu aishi kwa uwezo wake, kila mbuzi ashibe kwa urefu wa kamba yake.
 
Hii ni legacy ya Nyerere na sera zake za kipumbavu kama ujamaa

If we could go back in time ningetamani Kambona afanikiwe kupindua serikali ya Nyerere na kuintroduce capitalism from the 60s. Hii mentality ya kuombaonba hovyo kila ukiwa na shida isingekwepo.

Kila mtu aishi kwa uwezo wake, kila mbuzi ashibe kwa urefu wa kamba yake.
Kenya na ubepari bado wana harambee kule Ulaya na USA wako na fundraising wewe kapuku wa elimu jitahidi kuelewa

USSR
 
Screenshot_20210705-174418~3.png
 
Kenya na ubepari bado wana harambee kule ulaya na USA wako na fundraising wewe kapuku wa elimu jitahidi kuelewa

USSR
Ni kwa vitu muhimu vyenye manufaa kwa jamii, sio kila kitu

Nchi zenye utamaduni wa kibepari watu kuombaomba hovyo ni aibu na unapoteza heshima.

Hata mkienda lunch kama group kila mtu anajilipia.
 
Kama una mgonjwa anayehitaji fedha nyingi kwa ajili ya matibabu ntachangia,kama umekwama ada ntakuchangia,kama umepata msiba wa karibu ntakueezesha kidogo,ila kama ni harusi,kipaimara,graduation,birthday party,au sherehe nyingine yoyote ya anasa sitakuchangia!! Sitoi hata mia!
 
Mie nilijiwekea utaratibu wa kuchangia shida tu hizi starehe kila mtu apambane na hali yake. Ila sasa ndo inatokea ni rafiki au ndugu kabisa anaoa au kuolewa basi unaona huu msala sasa!![emoji2297][emoji2297][emoji2297]
Kama ndugu ntamchangia kiasi.Hizi kadi nyingine sichangi hata mia
 
Back
Top Bottom