Habari wadau,
Leo nimepata muda kujiuliza hivi hii tabia ya Watanzania (walio wengi) au jamii yetu kupenda sana tabia ya kuanzisha michango na kuchangia tumeipata wapi? Au ni ile toka enzi za siasa za ujamaa na kujitegemea?
Sipingi kuchangia mambo muhimu, ni jambo jema sana kuchangia mambo muhimu ya maendeleo.
Lakini hivi sasa tabia hii imezidi kwa kweli. Najua kuchangia si lazima ni hiari Lakini imekuwa too much!
Kila group la whatsup likianzishwa, wiki ya kwanza ya pili mchango. Wanasiasa kitu kidogo, wananchi tunaomba mchangie kidogo. Tabia hii mpka serikali kupitia viongozi wake, wanahamasisha michango, huku wakizitafuna kodi bila kujali.
Leo mtu anafungua kesi mahakamani ambayo haina gharama zozote zaidi anahamasisha umma umchangie.
Nina magroup ya whatsup takribani Matano baada ya kuyapunguza sana, lakini bado nikimaliza mchango huu, group lile linaleta michango miwili au zaidi. Matatizo ni yale yale.
Tupunguze haya mambo jamani.