Tabia ya Watanzania kupenda michango

Setting ikoje hiyo nami nifanye? Yani juzi kuna mtu nimempa namba kesho yake tayariii nipo group sijui jumuiya ya mtakatifu gani tayari anaomba michango nikabaki...,[emoji15]
Yaan sasa hivi namba za simu ni fursa...mtoto wa ukoo wa mbali utashangaa kakuunga kwenye group kume mwezi ujao anaoa[emoji848]
 

Wewe ni mpumbavu
 
Kiukweli hii michango ya sherehe inakera si kidogo, sasa unakaa unajiuliza huyu/hawa wameshtukizwa kufanya sijui send off sijui harusi? Maana kama umepanga kuoa/kuolewa hakuna haja ya kusumbua watu, angalia watu wako wa karibu + ndugu zako.....tena wamekuja na kautaratibu ka kuanzia 70 single laki double, jamani.....Yaani tupambane kuweka akiba bado tupambane na kusherehesha watu.

Halafu michango inakuwa kama deni vile, unawindwa hupumui.

Si lazima ujaze liukumbi, angalia idadi ya watu unaoweza kuafford chakula na vinywaji ....Wao wakija watakuja na zawadi...Ila budget iwe jukumu lako.
Watu 20 - 25 mbona sherehe inanoga tu.

Ugonjwa na misiba sawa.
 
Tunatakiwa tuanze kukataa kwa kutochanga. Yaani hata ukumbuni huwa sioni cha maana zaidi ya makelele ya maspika na mbwembwe za ma MC,yaani kwa kweli huwa sioni cha maana kinachofanyika
Kimasihala masihala milioni 30 zimetumika.
 
hivi na hii michango ya kuvhangia sijui majengo ya mashule, hospitals e.t.c ni kwa sheria ya wapi???
 
Umezaliwa lini? Mbona wakati wa nyerere hakukuwa na michango mingi? Kwanza kipindi hicho vitu kama harusi vilikuwa simple sana na hakukuwa na vikao vingi. Mambo ya michango yameanza kushika kasi tangu watu wajue kitu kinachoitwa ''whatsup''. Whatsup imerahisisha kuweka watu kwenye ma-group na kuombana michango kwa vitu hata vya kijinga. Njia moja kubwa ni kujitoa kwenye hayo ma-group na kubakiwa na yale unayoona yana umuhimu.
 
Hii ndiyo dawa. Na siku hizi wanawake wa uswazi wanajifanya kuwa wazungu kuliko hata wazungu wenyewe. Wengi hawajaenda shule hivyo wanakuwa rahisi sana kuingia kwenye mkumbo. Kitu kama birthday uswahilini imekuwa kama ni lazima. Kuna mama mmoja darasa la saba ukimsikia anavyozitamka sasa. Utasikia ''nilikuwa kwenye basi-dei ya jirani yangu''. Wamejua mpaka baby shower wewe unafikiria mchezo. Kweli ukitaka kujua gharama za ujinga nenda uswahilini huko uone kina mama wanavyoshindana na sherehe.
 
Tunatakiwa tuanze kukataa kwa kutochanga. Yaani hata ukumbuni huwa sioni cha maana zaidi ya makelele ya maspika na mbwembwe za ma MC,yaani kwa kweli huwa sioni cha maana kinachofanyika
Ni utopolo mtupu na kupotezeana muda na pesa.
 
Nimeachana na ujinga wa kujipa umaskini, nachangia kwenye mambo ya msingi kama majanga
 
Katika vitu siviruhusu Ni kupelekeshwa pasipo hiari ya maamuzi yangu (isipokuwa mume tu), kama mtu sitaki kumchangia napiga kimya, Sina group na kwa misimamo yangu sijui mtu kuniunga group bila kunijulisha anakuwa amejiamini nini,

Maisha raha sana ukipuuza kero ndogo ndogo
 
Harusi ni mzigo kwa wengine.hasa wale ambao hawachangagi kabisa kwa wenzao wao wanajua kudai hadi kero

Halafu,utakuta kuna gharama za kijinga zinazoongeza mzigo ,mfano ,wewe mwanaume unapewa kadi ya send off halafu mkeo anapewa kadi ya kitchen party.Haya mambo ya kitchen party ni ujinga mtupu.Yaani mtu mwingine ameshakaa na mume na kupata hadi wajukuu kabisa ,anaamua kubariki ndoa naye anataka afanyiwe kitchen party Huu ni ujinga plus
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…