Tabia ya Watanzania ya kuzaa hovyo ndiyo chanzo cha umaskini. Bodaboda ana watoto sita! Hata Serikali inashindwa kupanga mipango

Hukusikia wanaambiwa na rais wao wafyatue watoto? Kosa lao liko wapi wakati wanafuata ushauri wa viongozi ''majembe'' wa CCM?
 
Huo ni upumbavu.Kwani bila Serikali hawezi ishi???Huo ni udhalilishaji wa ubinadamu wake.Tatizo ni kupenda ngono boila kufanya kazi.Kama mtu anawajibika hawezi lalamikia Serikali yake.
Hiyo Ndio Pointi ......kupenda ngono. kazi wanafanya lakini kutokana na mazingira tofauti wengine vipato au uzalishaji bado ni Duni.

Mtu anayezalisha ni Mmoja kwenye familia ila watumiaji ni 8. Huyu hata afanye vipi hawezi kukidhi mahitaji
 
Trump ana 5......tajiri la kutupwa. Halafu boda ana 6.

George Bush anaye momoja tu, wewe wa kwa Mtogole unao 6.

Obama ana 2 tu....wewe kinyozi unao 8.

Bill Clinton anaye mmoja tu ...wewe muuza nyanyaunao 20
Nilikua Zanzibar kuna Guider mmoja chalii sana akaniambia ana wake wawili na watoto 8!! Nilishangaa sana.
 
Serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa sababu ndiyo yenye jukumu la kuongoza. Zamani kipindi cha Nyerere kulikuwa na chama cha uzazi na malezi bora Tannzania, na kilikuwa active sana. Ofisi kila mahali na watu walikuwa wanahimizwa kuzaa kwa mpango. Siku hizi raia wanaambiwa wafyatue watoto.
 
Hakuna, ni uongo.....hao unaoita wazee wenu ndio wametufikisha hapa na hii dhana ya kuzaa hovyo bila mipango wala mwelekeo ni utamaduni kutoka kwa wazee hao hao.
Kwani wewe unateseka na nini?Njaa?Elimu?Umaskini?Ujinga?Kansa?Ndoa?Kama hujaridhika na hali uliyo nayo hata ukipelekwa mbinguni bado utasema Mungu anakosea sana kwa sababu tu ya kukosa shukrani,kujiamini na kupambania kile unachokitafuta.
 
Kwani wewe unateseka na nini?Njaa?Elimu?Umaskini?Ujinga?Kansa?Ndoa?Kama hujaridhika na hali uliyo nayo hata ukipelekwa mbinguni bado utasema Mungu anakosea sana kwa sababu tu ya kukosa shukrani,kujiamini na kupambania kile unachokitafuta.
Mimi siteseki bali watoto wa hizo familia wanaishi maisha mabaya sana. Ni Uhai tu.
 
Nyie wenye pesa za Kulamba Asali pigeni kazi, fyatueni
Ni akili mgando kuamini kuwa kila mwenye pesa ni za kutoka CCM,mimi na hao walambisha asali ni ardhi na mbingu,tena ukinipeleka pande hizo unanivunjia adabu.
 
Nonesense
 
Mimi nipo tofauti na mtazamo wako, kuhusu kuzaa watoto ni Baraka toka kwa Mungu.

Ikiwa Mungu amekujalia kizazi basi zaa accordingly. Acha mawazo ya kusema kuhusu huduma n.k

Wazazi wako walipokuzaa wewe walikuwa hata na baiskeli ? Achilia mbali laki tano bank?

Mimi endapo Mungu ananibariki kupata mke mwema wa kunifaa maishani mwangu, sharti lq kwanza ni utayari wake kuhusu kuzaa.
Ni lazima awe na utayari wa kunizalia watoto wasiopungua wanne and maximum six kids.
Lakini swaga za kizungu eti mtoto mmoja au wawili tu, anipishe kabisa, sitokuwa tayari kuoa mwanamke wa hivyo kwa sababu mwisho wa siku atanipa majaribu ili nikatafute mwanamke mwingine nje ili anizalie mtoto.

Nitampenda sana mke wangu mpenzi LAKINI awe tayari kuhusu suala la kuzaa watoto na sio mtoto mmoja.
 
Umeongea ukweli mchungu sana ambao waafrika wengi zaidi hawapendi kuusikia.
 
Kuna namna unaelezaa vitu kwa uhalisia kbsaaa...nimependa hoja zakoo...watanzania ni wazembe wa kufikiri..Na ni wepesi wa kujifariji...kizazi bora kinatengenezwaa na sio neema za Mungu...tuache kujifariji dunia imebadilika...
Watz wao ni kuwa na majibu mepesi kwenye masuala ya msingi.
Utasikia "mipango ya mungu"
Ila jamani watz sie kweli chaneli ya comedy huko mbingini
 
Mimi siteseki bali watoto wa hizo familia wanaishi maisha mabaya sana. Ni Uhai tu.
Hapana ndugu yangu fanya utafiti vizuri maana watu ambao hawana familia yaani wamekosa majukumu wengi wao hali zao za maisha siyo nzuri maana akili yao inakuwa inatawaliwa na tamaa,kutokujiamini na starehe hivyo kusababisha kiwango kikubwa cha umaskini na utegemezi katika jamii.
 
Siyo kweli swali fikirishi je serikali ya CCM ina mpango wowote wa kuinua kipato cha mtu mmojammoja
 

Na hili ni tatizo mpaka leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…