Tabia ya Watanzania ya kuzaa hovyo ndiyo chanzo cha umaskini. Bodaboda ana watoto sita! Hata Serikali inashindwa kupanga mipango

Kwa mwendo huu hakuna Rais atakayeweza kuumaliza umaskini wa nchi hii.

Ili twende sawa nitoe tafsiri ya umaskini kwa mujibu wa IMF:- umaskini ni hali ya kukosa huduma za afya/maji, chakula, elimu na mahala pazuri pa malazi (nyumba bora).

Kwa tafsiri hii, na kwa uzazi holela wa hapa nchini, ni lini kila mtanzania atakuwa na uwezo wa kuwa na nyumba bora, uwezo wa kupata huduma za afya aitakayo kwa bima ama fedha yake, uwezo wa kupata milo 3 bila shida yoyote?

Unakuta bodaboda ana watoto 6? Mama ntilie, machinga na barmaid eti nao wana familia kubwa? Nchi hii tunaenda wapi? Watu waelimishwe kuwa, siyo kila mtu lazima azae. Watoto siyo asset kwamba utakopea mkopo.

Serikali ikijenga shule ama zahanati, miaka 2 tu zimezidiwa na idadi ya watu. Hata madawati yanakuwa tatizo kila mwaka kwasababu watanzania wanafyatua watoto mno. Hakuna kitu kinawezekana bila family planning.

Dkt. Slaa alipokuwa balozi Sweden alisema "Tanzania na Sweden zilikuwa na idadi sawa ya watu mwaka 1961 (milioni 9 kila moja). Hivi sasa Sweden ina watu 15M, wakati Tanzania ina watu 60+M". Hii ni hatari.

Kwa ujinga huu wa kuzaa hovyo umaskini hautatuachia. Watu milioni 60, walipa Kodi 2M !!!

Itungwe sheria, mtu akitaka kuzaa aweke milioni 10M benki kama dhamana ya malezi bora ya mtoto.

Vinginevyo, shika, peleka akafungwe.
Hukusikia wanaambiwa na rais wao wafyatue watoto? Kosa lao liko wapi wakati wanafuata ushauri wa viongozi ''majembe'' wa CCM?
 
Huo ni upumbavu.Kwani bila Serikali hawezi ishi???Huo ni udhalilishaji wa ubinadamu wake.Tatizo ni kupenda ngono boila kufanya kazi.Kama mtu anawajibika hawezi lalamikia Serikali yake.
Hiyo Ndio Pointi ......kupenda ngono. kazi wanafanya lakini kutokana na mazingira tofauti wengine vipato au uzalishaji bado ni Duni.

Mtu anayezalisha ni Mmoja kwenye familia ila watumiaji ni 8. Huyu hata afanye vipi hawezi kukidhi mahitaji
 
Trump ana 5......tajiri la kutupwa. Halafu boda ana 6.

George Bush anaye momoja tu, wewe wa kwa Mtogole unao 6.

Obama ana 2 tu....wewe kinyozi unao 8.

Bill Clinton anaye mmoja tu ...wewe muuza nyanyaunao 20
Nilikua Zanzibar kuna Guider mmoja chalii sana akaniambia ana wake wawili na watoto 8!! Nilishangaa sana.
 
Kuna mama niliona ana watoto 8 anamlilia Makonda amsaidie kuwalea 😄

Sasa unapiga mtoto wa kwanza mpk wa 8 unategemea nani aje awalee? Mwanaume akiona yamemzidi anakula kona 😄😄

Badae unailaumu serikali Maisha magumu 🙆🙆
Serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa sababu ndiyo yenye jukumu la kuongoza. Zamani kipindi cha Nyerere kulikuwa na chama cha uzazi na malezi bora Tannzania, na kilikuwa active sana. Ofisi kila mahali na watu walikuwa wanahimizwa kuzaa kwa mpango. Siku hizi raia wanaambiwa wafyatue watoto.
 
Hakuna, ni uongo.....hao unaoita wazee wenu ndio wametufikisha hapa na hii dhana ya kuzaa hovyo bila mipango wala mwelekeo ni utamaduni kutoka kwa wazee hao hao.
Kwani wewe unateseka na nini?Njaa?Elimu?Umaskini?Ujinga?Kansa?Ndoa?Kama hujaridhika na hali uliyo nayo hata ukipelekwa mbinguni bado utasema Mungu anakosea sana kwa sababu tu ya kukosa shukrani,kujiamini na kupambania kile unachokitafuta.
 
Mimi siteseki bali watoto wa hizo familia wanaishi maisha mabaya sana. Ni Uhai tu.
 
Nyie wenye pesa za Kulamba Asali pigeni kazi, fyatueni
Ni akili mgando kuamini kuwa kila mwenye pesa ni za kutoka CCM,mimi na hao walambisha asali ni ardhi na mbingu,tena ukinipeleka pande hizo unanivunjia adabu.
 
Usinilazimishe kuamini unachokijua hata kama kina faida kwako.Mimi siamini katika ujinga wa kuwa na watoto wawili ambao hauna faida kwangu.Mimi ni mjamaa ndiyo maana siamini katika kuzaa watoto wachache.Tumeona hasara yake kwa sisi wajamaa,kwanza Ushoga ni chanzo cha sera hizi za kuwa na watoto wachache,pili tunakoelekea thamani ya mwanaume itaendelea kushuka kwa sera hizi.Siku moja Putin aliwaasa Wanawake nchini kwake wazae sana na atawalipa mishahara kama watazaa sana ina maana wanaume wa huko hawana ngu za kuzaa.Yote haya yanatokana na mashinikizo ya kiuchumi,kielimu,kisiasa katika kugandamiza baraka ya Mwenyezi Mungu.(Mwanzo 1:26-29).
Nonesense
 
Mimi nipo tofauti na mtazamo wako, kuhusu kuzaa watoto ni Baraka toka kwa Mungu.

Ikiwa Mungu amekujalia kizazi basi zaa accordingly. Acha mawazo ya kusema kuhusu huduma n.k

Wazazi wako walipokuzaa wewe walikuwa hata na baiskeli ? Achilia mbali laki tano bank?

Mimi endapo Mungu ananibariki kupata mke mwema wa kunifaa maishani mwangu, sharti lq kwanza ni utayari wake kuhusu kuzaa.
Ni lazima awe na utayari wa kunizalia watoto wasiopungua wanne and maximum six kids.
Lakini swaga za kizungu eti mtoto mmoja au wawili tu, anipishe kabisa, sitokuwa tayari kuoa mwanamke wa hivyo kwa sababu mwisho wa siku atanipa majaribu ili nikatafute mwanamke mwingine nje ili anizalie mtoto.

Nitampenda sana mke wangu mpenzi LAKINI awe tayari kuhusu suala la kuzaa watoto na sio mtoto mmoja.
 
Kwa mwendo huu hakuna Rais atakayeweza kuumaliza umaskini wa nchi hii.

Ili twende sawa nitoe tafsiri ya umaskini kwa mujibu wa IMF:- umaskini ni hali ya kukosa huduma za afya/maji, chakula, elimu na mahala pazuri pa malazi (nyumba bora).

Kwa tafsiri hii, na kwa uzazi holela wa hapa nchini, ni lini kila mtanzania atakuwa na uwezo wa kuwa na nyumba bora, uwezo wa kupata huduma za afya aitakayo kwa bima ama fedha yake, uwezo wa kupata milo 3 bila shida yoyote?

Unakuta bodaboda ana watoto 6? Mama ntilie, machinga na barmaid eti nao wana familia kubwa? Nchi hii tunaenda wapi? Watu waelimishwe kuwa, siyo kila mtu lazima azae. Watoto siyo asset kwamba utakopea mkopo.

Serikali ikijenga shule ama zahanati, miaka 2 tu zimezidiwa na idadi ya watu. Hata madawati yanakuwa tatizo kila mwaka kwasababu watanzania wanafyatua watoto mno. Hakuna kitu kinawezekana bila family planning.

Dkt. Slaa alipokuwa balozi Sweden alisema "Tanzania na Sweden zilikuwa na idadi sawa ya watu mwaka 1961 (milioni 9 kila moja). Hivi sasa Sweden ina watu 15M, wakati Tanzania ina watu 60+M". Hii ni hatari.

Kwa ujinga huu wa kuzaa hovyo umaskini hautatuachia. Watu milioni 60, walipa Kodi 2M !!!

Itungwe sheria, mtu akitaka kuzaa aweke milioni 10M benki kama dhamana ya malezi bora ya mtoto.

Vinginevyo, shika, peleka akafungwe.
Umeongea ukweli mchungu sana ambao waafrika wengi zaidi hawapendi kuusikia.
 
Kuna namna unaelezaa vitu kwa uhalisia kbsaaa...nimependa hoja zakoo...watanzania ni wazembe wa kufikiri..Na ni wepesi wa kujifariji...kizazi bora kinatengenezwaa na sio neema za Mungu...tuache kujifariji dunia imebadilika...
Watz wao ni kuwa na majibu mepesi kwenye masuala ya msingi.
Utasikia "mipango ya mungu"
Ila jamani watz sie kweli chaneli ya comedy huko mbingini
 
Mimi siteseki bali watoto wa hizo familia wanaishi maisha mabaya sana. Ni Uhai tu.
Hapana ndugu yangu fanya utafiti vizuri maana watu ambao hawana familia yaani wamekosa majukumu wengi wao hali zao za maisha siyo nzuri maana akili yao inakuwa inatawaliwa na tamaa,kutokujiamini na starehe hivyo kusababisha kiwango kikubwa cha umaskini na utegemezi katika jamii.
 
Kwa mwendo huu hakuna Rais atakayeweza kuumaliza umaskini wa nchi hii.

Ili twende sawa nitoe tafsiri ya umaskini kwa mujibu wa IMF:- umaskini ni hali ya kukosa huduma za afya/maji, chakula, elimu na mahala pazuri pa malazi (nyumba bora).

Kwa tafsiri hii, na kwa uzazi holela wa hapa nchini, ni lini kila mtanzania atakuwa na uwezo wa kuwa na nyumba bora, uwezo wa kupata huduma za afya aitakayo kwa bima ama fedha yake, uwezo wa kupata milo 3 bila shida yoyote?

Unakuta bodaboda ana watoto 6? Mama ntilie, machinga na barmaid eti nao wana familia kubwa? Nchi hii tunaenda wapi? Watu waelimishwe kuwa, siyo kila mtu lazima azae. Watoto siyo asset kwamba utakopea mkopo.

Serikali ikijenga shule ama zahanati, miaka 2 tu zimezidiwa na idadi ya watu. Hata madawati yanakuwa tatizo kila mwaka kwasababu watanzania wanafyatua watoto mno. Hakuna kitu kinawezekana bila family planning.

Dkt. Slaa alipokuwa balozi Sweden alisema "Tanzania na Sweden zilikuwa na idadi sawa ya watu mwaka 1961 (milioni 9 kila moja). Hivi sasa Sweden ina watu 15M, wakati Tanzania ina watu 60+M". Hii ni hatari.

Kwa ujinga huu wa kuzaa hovyo umaskini hautatuachia. Watu milioni 60, walipa Kodi 2M !!!

Itungwe sheria, mtu akitaka kuzaa aweke milioni 10M benki kama dhamana ya malezi bora ya mtoto.

Vinginevyo, shika, peleka akafungwe.
Siyo kweli swali fikirishi je serikali ya CCM ina mpango wowote wa kuinua kipato cha mtu mmojammoja
 
Ukisoma kitabu cha "Building a Peaceful Nation: Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanzania 1960-1964" Dr. Paul Bjerk ameandika jinsi serikali ya kwanza kabisa ya Nyerere ilipojitahidi kufanya mipango mizuri sana ya maendeleo, lakini tatizo likawa kuwa serikali haikuangalia ongezeko la watu.

Mipango ya miaka mitano ikikamilika, inakuwa haijamaliza tatizo, kwa sababu by the time miaka mitano inaisha, idadi ya watu ineshaongezeka na kuipita sana mipango.

Na hili ni tatizo mpaka leo.
 
Back
Top Bottom