Tabia ya Watanzania ya kuzaa hovyo ndiyo chanzo cha umaskini. Bodaboda ana watoto sita! Hata Serikali inashindwa kupanga mipango

Tanzania tuna hasara Sana ... Ndiomaana population tegemezi haipungui,,, ukiona nchi zaidi ya 45% niwatoto haiwezi kuendelea kamwe
Ni kweli maendeleo ya Taifa yanaanza na mtu mmoja mmoja kwenye ngazi ya Familia.

Sasa huku ndio choka mbaya.

Mzalishaji mmoja watumiaji 10.
 
Wacha watu wazae vije vizazi vipya vya kuikomboa Tanzania Kama China na Nigeria. Sio kizazi hichi cha Simba na yanga pumbavu zako mwana Ccm wewe.
Watakuwa wakombozi wanaopatikana kwa Bahati na sibu otherwise maandalizi ni muhimu.
 
Kuzaa na kupata watoto sio tatizo. Tatizo ni kuzaa bila kuandaa mipango ya namna watoto wataishi. Tusipozaliana miaka 20 au 30 ijayo tutaanza kupata gepu la idadi ya nguvu kazi. Watu wengi watakuwa ni wazee vijana active watakuwa ni wachache.

Wazazi wetu walituzaa 5 hadi 12 kwa wastani katika familia zetu. Siku hizi wastani ni watoto 1 hadi 3. Hii ni mbaya sana. Na hawa 1 hadi watatu tunawapata umri umeenda sana kuanzia miaka 30+ hii ni hatari sana kwa ustawi wa jamii.

Mataifa ya magharibi wanataka tusizaliane ili idadi ya watu ipungue iwe chini wao waje kusomba rasilimali. Tukiwa wachache ni rahisi wao kurubuni viongozi wetu kutupatia misaada isiyo na riba wakijifanya ni kusaidia kumbe ile misaada inatufanya tusahau kabisa kuwa kuna kesho na tunaridhika nayo huku wao nyuma ya pazia wakisaini mikataba ya kuhodhi rasilimali zetu kama madini, mafuta, gesi na kadhalika kwa urahisi kabisa.

Tushtuke na tuwe makini. Taifa lolote ili kuendelea linahitaji idadi ya watu kuongezeka na wingi wa watu ndio chachu ya kuboost matumizi sahihi ya rasilimali.

Tazama mataifa yanayopiga hatua kwa kasi kama India, china, Nigeria. Yana sifa gani ambayo ni common, si idadi kubwa ya watu?

Wewe leo taifa gani kubwa litakwenda India au china kutaka wachimbe rasilimali zao na watu ni wengi vile wanashida hadi kwenye kucha?

So msidanganyike, wazungu kwanza wao wana low birth rate kwasasa ndio maana wanahofu taifa kubwa kama afrika linavyozaliana kwa kasi na wametudhurumu sana rasilimali zetu tokea miaka yote tukisimama tutawafanya nini siku za baadae. Walimchekea mchina leo tazama anavyowakimbiza kiuchumi na ni juzi tu hapo alikuwa kataifa ka hovyo. Leo afrika ikisimama itakuwaje?

Sasa itasimamaje na watu wanaoogopa kuzaliana kwa wingi unaotakiwa?
 
Hauna uelewa na unachozungumzia,,, kwanza unatakiwa kufaham zaidi ya 43% niwatoto chini ya miaka 15, wengine Kati ya Mika 15- 20 ambao kimsingi bado hajaweza kuzalisha kiyu Ni zaidi ya 10% Wazee Ni juu ya 7% bado hapo Kuna asilimia za vijana wa hovyo ,, hii Ina manaa zaidi ya 60% ya idadi ya watu Tanzania ni tegemezi ,, Taifa Kama hili halitaweza kujitegemea,, lazima kuwepo na juhudi za makusudi za kuwa na sera ya kuzaa watoto wawili ili kuwe na Uwiano sawa hata watatu itasaidia sana
 
Sisi wenye uwezo wacha tuzalishe tu maana mashoga wanaongezeka kwa kasi ya ajabu tukileta uzungu wa kuzaa watoto wawili tumekwisha.
Zaa hata watoto 20 kama uwezo wa kuwatunza unao ila km huna uzizalishe ukitegemea serikali ikuleleke mtoto wako
 
We ni mgumba!? Tuanzie hapo kwanza maana si kwa chuki hizo.
 
Kama ni baraka za mungu kwanini usizae watoto kumi? Na sio hao wanne?
 
Huwa mnanichosha mnapozitaja india na nigeria eti ni nchi zilizopiga hatua kiuchumi! Ilhali ni nchi zenye umaskini wa kutupwa yaani ni shithole countries...hiyo china yenyewe almost robo tatu ya watu wake ni maskini wa kutupwa.

Mi ninachosema tuzae ili tuwe na mipango kuhakikisha vizazi vyetu vinakuja kuwa na faida kwa nchi. Hali kama hairuhusu zaa watoto wawili tu kujipunguzia mzigo na kuipunguzia mzigo serikali
 
Kwani kuna nchi serikali inalea watoto wa raia zake? Ninaposema uwezo ni pamoja na kulea. Au wewe umeelewa vipi?
Serikali inasaidia malezi ya mtoto wako au wewe hujui hilo?

Kuanzia shule, hospital na miundo mbinu yote unayoiona ni sehemu ya malezi ya mtoto wako!

Au unafikiri malezi mpaka serikali imchukue iishi nae ndio ujue kwamba inamlea?
 
Hata kama raia tungekua milioni moja kama wanao tawala ni ccm bado nchi ingekua maskini tuu mfumo mbovu wa kiutawala usioleta usawa kwa watu ndio sababu ya ugumu maisha ya Watanzania wengi, tuaache watu tuchape mkia ni maisha yetu tutajua sisi wataishi vipi watasoma vipi wewe zaa kizungu usitupangie chakufanya
 
Serikali inasaidia malezi ya mtoto wako au wewe hujui hilo?

Kuanzia shule, hospital na miundo mbinu yote unayoiona ni sehemu ya malezi ya mtoto wako!

Au unafikiri malezi mpaka serikali imchukue iishi nae ndio ujue kwamba inamlea?
Usiniletee kichefuchefu mimi watoto wangu wote nimesomesha kwa hela yangu kuanzia kindergarten hadi University bila mkopo hivyo hizo ngonjera zako sizielewi na ninaelewa ninachozungumza.
 
Itungwe sheria, mtu akitaka kuzaa aweke milioni 10M benki kama dhamana ya malezi bora ya mtoto.

Vinginevyo, shika, peleka akafungwe.
Hahaha..
Kwa mtindo huo si serikali italazimika kuwekeza massively kwenye idara ya magereza, maana walala hoi a.k.a "wanyonge" karibu wote itabidi wahamishie makazi Lupango!

Pia kumbuka kuna dini inayohamasisha wafuasi kuzaa sana, hata kiholela, ili tu kuongeza idadi ya waumini wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…