Tabia za matajiri wa kibongo zinafanana

Nduka Original

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
1,012
Reaction score
817
Matajiri wa kibongo wote wanatabia sawa kama umeshapata bafasi ya ku deal nao kibishara.

1. Wote ni waongo - atakuambia atakulipa siku fulani ila haitatokea
2. Wote ni warushi - atahakikisha katika biashara anakurusha ka kiasi fulani
3. Wote wana wivu - hawataki kabisa tulioko chini tuwasogelee ndio maana wanawake hila katika biashara
4. Wote wana roho mbaya - hawajali kabisa wewe kupoteza jasho lako anajuwa huna cha kumfanya
5. Wote ni wababe - Atakulalia sana akijuwa huna cha kumfanya
6. Kuchafua jina - Siku akikurusha yeye ndio anakuchafuwa jina kwa matajiri wenzake

Wanapenda waonyeshe utajiri wao sehemu za matumizi kama bar kwenye migahawa kwa ujumla, sasa fanya nao biashara uone ni vituko vitupu - full usanii
 
Mh! Sijui ngoja tusikie kutoka kw watu wanaodeal nao direct
 
7 - Asilimia kubwa pesa zao wamezipata kwa njia zisizo halali. (kuiba, hirizi nk)
8 - Wengi wao hukwepa kulipa kodi.
9 - Wengi wao ni watoaji rushwa wakubwa
10 - Wengi wao ni vigumu kuingia katika ufalme wa Mungu kuliko ngamia ktk tundu la sindano.
 
sina cha kuongeza ila na-compile tu majibu yenu.
1. Wote ni waongo - atakuambia atakulipa siku fulani ila haitatokea
2. Wote ni warushi - atahakikisha katika biashara anakurusha ka kiasi fulani
3. Wote wana wivu - hawataki kabisa tulioko chini tuwasogelee ndio maana wanawake hila katika biashara
4. Wote wana roho mbaya - hawajali kabisa wewe kupoteza jasho lako anajuwa huna cha kumfanya
5. Wote ni wababe - Atakulalia sana akijuwa huna cha kumfanya
6. Kuchafua jina - Siku akikurusha yeye ndio anakuchafuwa jina kwa matajiri wenzake

Wanapenda waonyeshe utajiri wao sehemu za matumizi kama bar kwenye migahawa kwa ujumla, sasa fanya nao biashara uone ni vituko vitupu - full usanii

7 - Asilimia kubwa pesa zao wamezipata kwa njia zisizo halali. (kuiba, hirizi nk)

8 - Wengi wao hukwepa kulipa kodi.
9 - Wengi wao ni watoaji rushwa wakubwa
10 - Wengi wao ni vigumu kuingia katika ufalme wa Mungu kuliko ngamia ktk tundu la sindano.
 
chezea utajiri wewe!!!!:violin:
 
Ungependa uwe tajiri siku moja? Nahisi unachukia utajiri wewe! Hahahaaaa! Huo ni uchaguzi wako kubaki ulivyo. Kuchukia matajiri ni kuchukia utajiri. Kama unandoto nawe uwe tajiri penda matajiri, penda njia zao utajifunza uwe kama walivyo kisha nawe utatesa. Jambo lolote lile ukishalichukia kamwe haliwezi nalo likakupenda, utazidi kuwa mbali nalo! Kuchukia matajiri ni kuchagua umasikini ni kuchagua mateso duniani.

Dini zimeturoga masikini tuchukie utajiri wakati viongozi wa dini ni matajiri na wanaishi kwenye Kasri, wanafanya watu kuchukia matajiri na utajiri eti wanafundisha kwamba HERI walio MASIKINI duniani maana ufalme wa mbinguni ni wao! Kwamba ni rahisi ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia mbinguni! Kwa hiyo Ulaya yote, Marekani na Uarabuni wote watakwenda motoni na sisi masikini waaafrika tuchekelee maana tukifa mbingu ni yetu ata kama mbu wanatuuma leo kwa kushindwa kununua net, tunaharisha kwa kunywa maji machafu, tunashindwa kusomesha watoto kwa kukosa hela, tunashindwa kujitibia, barabara mashimo tu, njaa haiishi pamoja na kwamba tunaishi kando ya mito! Hahaaa matajiri watakiona mbinguni wakati masikini wanapeta!! Tazama na upande wa pili wa matajiri ili uwapende uweze kushiriki vita ya kupigana na dhambi ya umasikini! Hatuwezi kujikwamua iwapo hatutajifunza kitu kwa matajiri maana matajiri wote duniani wanafanya yale yale ambayo masikini hawafanyi kiasi kwamba mataifa mengine ni tajiri na mengine ni masikini! Matajiri wote wananidhamu fulani. Usitazame mabaya ya matajiri tu wanamazuri mengi ikiwamo kutoa ajira, hata masikini wanamabaya yao kwa mfano ni wahalifu sana, hahahahahaaaaa !!
 
Hizo bila kuwa nazo huwezi kuwa Tajiri, Ni lazima uwe na wivu, wewe huoni Samsung na I phone vitu wanafanyiana? Ni lazima Uchukie Competitors wako wote, mi i huwa nashangaa sana unaweza pita mtaani ukakuta maduka yamepangana na wote wanauza bidhaa moja na unawakuta wamekaa pamoja wanapiga story sema tu ni kwa sababu ni Biashara ya Uchuuzi,

Huwezi kuta Cocal na Peps wakiwa pamoja kila mtu yuko bise kutafuta njia za kumangamiza mwenzake na kumuondoa kabisa sokoni

Uongo nao ni Muhimu sana na hii ni Dunia nzima makampuni mengi ni waongo unatengenezewa simu unaelewa vitu vingine ambayo hata havipo, so bila uongo huwei fanya biashara

Na Mfanya kazi siku zote wewe ni mtumwa wa Tajiri, usitegemee Tajiri akuendeleze uwe kama yeye hakuna kitu cha aina hiyo Chini ya Jua
 
Uongo na urushi kwa kweli naunga mkono me cijui hawa watu wanakuwa nini yani utakuta unamdai pesa tena kidogo utavyozungushwa na mengine dharau juu.
 
Wengi wao ni vitajiri uchwara...after sometimes vinachacha sana!!!

Itakuwa applicable kama matajiri ni kwa level ya mmilki wa duka, salon, daladala, mashine ya kusaga, fundi mason / kujenga na tajiri yake anemjengea nyumba n.k yaani zile huduma ambazo mmilki ana interact moja kwa moja na mfanyakazi wake. lakini kwa ambae anamilki kampuni kampuni kubwa ambayo ina management yake mpaka akuonee wivu wewe atakuona wapi maana ukimuuliza wafanyakazi wake hajui kwa majina wala sura sana sana anawajua kwa idadi ya wanaume wangapi na wanawake wangapi basi
 
hizo pesa unazozitaja eti zina nguvu duniani sio kweli zina nguvu huko TZ ...kwenye moja ya nchi masikini sana duniani...huwezi enda na oman dinar hapo london ikaonekana ina thamani...dollar mnyamwezi ndo mwisho wa maneno yote...
 
Mi siamini kama bongo kuna matajiri kama wapo ni wachache sana..wengi ni waizi wa waziwazi na madhulumat tu.
 
Wengi wao ni waarabu, wachaga, wakinga, wahaya, waukuma na wapare
 
Mkuu umemaliza! Kuna ukweli flani kwenye maelezo yako
 
Hapana, tatizo la masikini wa Tanzania wanadhani ukiwa na pesa basi unatakiwa kuwagawia bure bure, sina pesa lakini nadhani ni busara kusubiri pesa sawia na jasho nimevulia. Ukiogopa wenye pesa katu huwezi pata pesa milele ustabaki kulalama matajiri wa kibongo wana sifa so and soo!
 
wapi mtoa mada aliposema anachukia matajiri???????ni hoja tu binafsi
 
hizo pesa unazozitaja eti zina nguvu duniani sio kweli zina nguvu huko TZ ...kwenye moja ya nchi masikini sana duniani...huwezi enda na oman dinar hapo london ikaonekana ina thamani...dollar mnyamwezi ndo mwisho wa maneno yote...

Ni kweli, umenikumbusha kisa kimoja niliwahi kutoa dola kununua kitu fulani kwenye maduka yaliyo nje kidogo ya Heathrow terminal4, muhudumu wa duka aliniuliza kwa jeuri "hii kitu gani?" nenda katafute hela inayojulikana! Jibu hilo nilichoka - Mataifa mengine yanajari sana thamani ya hela yao.!
 
wapi mtoa mada aliposema anachukia matajiri???????ni hoja tu binafsi
JF is the home of great thinkers, kama huoni wapi mtoa mada aliposema anachukia matajiri hilo ni tatizo lako binafsi !!!!! !!!! kama wengine nao hawaoni kama wewe basi hlo ni tatizo langu binafsi!!!!! Fikiria mtu aje akuchambue wewe maubaya yako kama alivyochambuliwa tajiri utaona unapendwa? kama unagombea ubunge akaja mtu kumwaga maubaya yako namna ile hadi ukakosa kuupata ubunge utasema sioni mtoa mada aliposema ananichukia mimi kugombea ubunge, lol, ni mawazo yangu tu yasikunyime usingizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…