Tabia za wakulima zinazosababisha kilimo kisiendelee

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Bila kupoteza muda zifuatazo ni tabia za wakulima zinazofanya kilimo kisiendelee:-

1. Kulima bila kufanya maandalizi
Wakulima wengi hawafanyi maandalizi mapenda yaani wanasubiri mvua inyeshe ndo waanze kusafisha shamba,kutafta mbegu na mbolea.Matokeo yake wanaelemewa na kazi au kushindwa kuhudumia shamba kikamilifu.

2. Wanasuburi taarifa za kitaalamu ziwafuate nyumbani
Wakulima wengi hawapendi kujiongeza kufuata taarifa za kitaalamu kwa kupiga simu au kufuata taarifa sahihi kwenye vituo vya utafiti hata km viko jirani yao. Wamebaki kulaumu eti wataalamu hawawatembelei utadhani wakivuna mazao watagawana.

3. Kulima kwa mazoea
Hata km wakishauriwa vipi, wakulima wa kitanzania ni wagumu mno kubadilika. Mfano wengi wameng'ang'ania kulima mahindi wakati mbolea bei iko juu mno wakati uzalishaji wa Alizeti na maharage ni "cheap".

4. Kulima bila malengo
Wakulima wengi hawalimi kwa malengo.Unakuta msimu wa mvua unaanza mkulima hajui atalima nini na kwa kiasi gani. Yaani bora liende.

5. Kulima bila kuzingatia soko
Alime nini kwa wakati gani na atamuuzia nani? Mtu anajilimia tu bila kujua atauza wapi.

6. Kulima kwa kuigana
Ikitokea mtu kalima nyanya akauza vizuri basi wote wanakimbilia kwenye kilimo cha nyanya. Matokeo yake ni nyanya kulimwa kwa wingi na kukosa soko.

Ni hayo tu.
 
Wakulima wengi hawafanyi maandalizi mapenda yaani wanasubiri mvua inyeshe ndo waanze kusafisha shamba,kutafta

ASANTE KWA TAARIFA
 
Ila sio kwamba wewe ndio una maono mazuri. Unaandika uko karibu na laptop au smartphone. Toka nje ujionee upepo na radi
 
Nimeandika huu uzi nikiwa natoka shamba kuvuna mahindi, so hata mimi ni mkulima
 
... hiyo ndio inaitwa subsistence farming kind of agrarian economy. Lengo hasa huwa mlo wa kujikimu familia isife njaa.

By the way hatuna farmers rather we have peasants and that's how peasantry works!
 
Bila kupoteza muda zifuatazo ni tabia za wakulima zinazofanya kilimo kisiendelee:-

1. Kulima bila kufanya maandalizi
Wakulima wengi hawafanyi maandalizi mapenda yaani wanasubiri mvua inyeshe ndo waanze kusafisha shamba,kutafta mbegu na mbolea.Matokeo yake wanaelemewa na kazi au kushindwa kuhudumia shamba kikamilifu.

2. Wanasuburi taarifa za kitaalamu ziwafuate nyumbani
Wakulima wengi hawapendi kujiongeza kufuata taarifa za kitaalamu kwa kupiga simu au kufuata taarifa sahihi kwenye vituo vya utafiti hata km viko jirani yao. Wamebaki kulaumu eti wataalamu hawawatembelei utadhani wakivuna mazao watagawana.

3. Kulima kwa mazoea
Hata km wakishauriwa vipi, wakulima wa kitanzania ni wagumu mno kubadilika. Mfano wengi wameng'ang'ania kulima mahindi wakati mbolea bei iko juu mno wakati uzalishaji wa Alizeti na maharage ni "cheap".

4. Kulima bila malengo
Wakulima wengi hawalimi kwa malengo.Unakuta msimu wa mvua unaanza mkulima hajui atalima nini na kwa kiasi gani. Yaani bora liende.

5. Kulima bila kuzingatia soko
Alime nini kwa wakati gani na atamuuzia nani? Mtu anajilimia tu bila kujua atauza wapi.

6. Kulima kwa kuigana
Ikitokea mtu kalima nyanya akauza vizuri basi wote wanakimbilia kwenye kilimo cha nyanya. Matokeo yake ni nyanya kulimwa kwa wingi na kukosa soko.

Ni hayo tu.
Hilo tatizo sio la wakulima tu pekee, nafikiri ni tatizo la watanzania tuliowengi. Ukianzisha biashara ya mgahawa ikatiki usishangae baada ya muda kdg kila kona kwny mtaa wako kuna mgahawa. Ukija makazini (especially ofisi za umma) kufanya kazi kwa mazoea ndo zao, kujiongeza na tuubunifu twa hapa na pale walaa!
Mwanafunzi kusoma akiwa hajui akimaliza anapata wap ajira, au ataenda kufanya kazi wap, anakuja kukumbuka hilo akisha graduate...
Nafikiri tubadili tu hz mindset zetu.
 
Ila sio kwamba wewe ndio una maono mazuri. Unaandika uko karibu na laptop au smartphone. Toka nje ujionee upepo na radi
Yupo sahihi Mkuu Mimi mwenywe ni mtoto wa mkulima nimeyashuudia wazizi wangu na wakulima wengine ndio kilimo Chao huko.
Anachoongea ndio kinachoendelea kwa wakulima wengi watu wanajilimia tu na ukijaribu kuwashauri utaambiwa wewe ni mtoto wa juzi hujui kitu kwenye kilimo ,Tena kama umesoma utaambiwa unaleta ujuaji
 
Back
Top Bottom