Tabia zinazoudhi na kukera mbele za watu

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
3,607
Reaction score
9,430
Wasalaam,

Moja kwa moja kwenye mada, Kuna baadhi tabia ambazo huwa tunazifanya mbele za watu lakini Ni mbovu na zinakera!

Mfano

1. Mtu yupo bize anatembea anakula, may be kanunua Hindi la kuchoma, ndizi, sambusa n.k ! Sawa njaa imekubana, huwez kukaa mahali hata Kama Ni kibandani ule ukimaliza uendelee na safari?

2. Kuongea na simu kwa sauti kubwa "kuropoka"

3. Mtu anatoka msalani huku anajiweka sawa, kuchomekea, kufunga zipu au kuweka sket sawa, kwani ulishindwa kujiweka sawa ndo utoke ?

4. Mpo mezani mmeagiza mfano nyama choma n.k, mzigo umeshakuja mezani, mtu hajanawa anachukua kinyango anaonja!

5. Mtu anamuona mtu anaemfahamu kwa mbali, anaanza kupiga makelele kumsalimia, kumpungia mkono haitoshi ? Salamu zenu zisumbue watu wengine?

6. Mpo buchani kukunua nyama, mteja anaishika nyama kwa mikono nikatie hapa! Tuna uhakika gani mikono yako ni salama na Safi?

7. Kujichokonoa meno kila saa! Mpaka tujue umetoka kula nyama?

8. Kurusha mate wakati wa kuongea, najua hii Ni unconditional, lakini ukijijua upo hivo jiepushe kumsogelea Sana mtu wakati wa mazungumzo , pia ebuka kuongea Sana 'kupayuka'

9. Kujifanya mjuaji kila mada unachangia na unakuwa main speaker. Siasa umo, dini umo, mpira umo kila kitu!

10. Mtu yupo bize barabarani au kwenye kadamnasi alafu simu Yake ameweka mziki Hana habari! Kwa faida ya Nani? Kama unapenda mziki vaa earphones.

Tuendelee kutiririka tabia mbaya zinazoudhi mbele za watu ambazo tunazichukulia tu kawaida!
 
Mtu yupo bize anatembea anakula, may be kanunua Hindi la kuchoma, ndizi, sambusa n.k ! Sawa njaa imekubana, huwez kukaa mahali hata Kama Ni kibandani ule ukimaliza uendelee na safari ?
Tabia inayonikera ni mimi kunikataza kula huku natembea vyakula ambavyo hata havihitaji mimi kunawa.

Yani nakula hindi ambalo halihitaji maji ya kunawa wala kijiko wala stiki unataka nikae dk 15 nzima napoteza kula mhindi tu.

Acha GUBU mkuu,mtataka hadi karanga tukae chini tule.Kuna vitu huwezi kula unatembea kama vile ugali wako umeweka kwenye sahani ni ngumu kula unatembea.

Au wali wako kwenye sahani ni ngumu kula huku unatembea.

Ukiona mtu anakula huku anatembea ujue yuko comfortable kula anatembea.
 
Sasa c uwe unatoka ili usikereke 😳😳😳
 
Kula Ni starehe mkuu,,, unahitaji utulivu ule umalize uendelee na shughuli zako !!!! Unapitaje barabaran unatafuna andaz, muwa, au mhindi ?
 
Kula Ni starehe mkuu,,, unahitaji utulivu ule umalize uendelee na shughuli zako !!!! Unapitaje barabaran unatafuna andaz, muwa, au mhindi ?
Acha gubu mkuu😀.

Kuna vyakula ambavyo ukila ile rate yake ya kuingia mwilini ni kubwa kidogo kama matonge ya ugali na wali ama vyakula vingine vizito kama hivi.

Sasa karanga,mahindi sio vyakula vizito hata kidogo.


Kula Ni starehe mkuu
Sasa wengine starehe yao ni kula wanatembea kwa vyakula vidogo vidogo kama hivyo.

Mi kama nna ruti yangu kutoka magomeni kanisani mpaka magomeni kwa mguu basi nanunua karanga zangu za mia nne huku natembea mdogo mdogo.

Sasa kuna vitu sio vya kukereka kabisa.
 
Kula Ni starehe mkuu,,, unahitaji utulivu ule umalize uendelee na shughuli zako !!!! Unapitaje barabaran unatafuna andaz, muwa, au mhindi ?
Inaweza kuwa ndio starehe yake kula huku anatembea

Ama kila starehe ni lazima uifanye ukiwa umetulia?
 
Mtu kuniona nakula muhindi huku natembea asiniambie ....aje kuniandika huku JF.
😐
 
Mtu anayetafuna kama panya au nguruwe..khaa!!

Mtu anayebeua ovyo..sawa kubeua hakuepukiki lakini unabeua kwa staha Jamani...hata kusema excuse me!!!!..loh!! Nachefukwa na watu wa ivyo
 
Mtu anayetafuna kama panya au nguruwe..khaa!!

Mtu anayebeua ovyo..sawa kubeua hakuepukiki lakini unabeua kwa staha Jamani...hata kusema excuse me!!!!..loh!! Nachefukwa na watu wa ivyo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…