kitalembwa
JF-Expert Member
- Jul 12, 2014
- 3,607
- 9,430
Wasalaam,
Moja kwa moja kwenye mada, Kuna baadhi tabia ambazo huwa tunazifanya mbele za watu lakini Ni mbovu na zinakera!
Mfano
1. Mtu yupo bize anatembea anakula, may be kanunua Hindi la kuchoma, ndizi, sambusa n.k ! Sawa njaa imekubana, huwez kukaa mahali hata Kama Ni kibandani ule ukimaliza uendelee na safari?
2. Kuongea na simu kwa sauti kubwa "kuropoka"
3. Mtu anatoka msalani huku anajiweka sawa, kuchomekea, kufunga zipu au kuweka sket sawa, kwani ulishindwa kujiweka sawa ndo utoke ?
4. Mpo mezani mmeagiza mfano nyama choma n.k, mzigo umeshakuja mezani, mtu hajanawa anachukua kinyango anaonja!
5. Mtu anamuona mtu anaemfahamu kwa mbali, anaanza kupiga makelele kumsalimia, kumpungia mkono haitoshi ? Salamu zenu zisumbue watu wengine?
6. Mpo buchani kukunua nyama, mteja anaishika nyama kwa mikono nikatie hapa! Tuna uhakika gani mikono yako ni salama na Safi?
7. Kujichokonoa meno kila saa! Mpaka tujue umetoka kula nyama?
8. Kurusha mate wakati wa kuongea, najua hii Ni unconditional, lakini ukijijua upo hivo jiepushe kumsogelea Sana mtu wakati wa mazungumzo , pia ebuka kuongea Sana 'kupayuka'
9. Kujifanya mjuaji kila mada unachangia na unakuwa main speaker. Siasa umo, dini umo, mpira umo kila kitu!
10. Mtu yupo bize barabarani au kwenye kadamnasi alafu simu Yake ameweka mziki Hana habari! Kwa faida ya Nani? Kama unapenda mziki vaa earphones.
Tuendelee kutiririka tabia mbaya zinazoudhi mbele za watu ambazo tunazichukulia tu kawaida!