Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Figo hufanya kazi muhimu kwenye miili yetu kama kuondoa sumu, kuchuja damu na kufyonza madini. Uharibifu wa figo unaweza usigundulike kwa miaka mingi kwa maana figo huweza kufanya kazi hata kwa 20% ya uwezo wake
Tabia zinazoweza kuharibu figo zako:
Kutokunywa maji ya kutosha. Mafigo huhitaji maji ya kutosha ili kufanya kazi zake kwa ufanisi. Kutokunywa maji ya kutosha kunaweza kusababisha sumu kukusanyika kwenye damu.
Kubana mkojo mara kwa mara huongeza mgandamizo wa mkojo kwenye figo na inaweza kusababisha mawe kwenye figo hata kupelekea figo kushindwa kufanya kazi zake vizuri.
Ulaji chumvi nyingi kwenye chakula. Watu wengi hutumia chumvi nyingi kuliko mahitaji ya mwili kitu kinachosababisha figo kuelemewa hivyo kupandisha shinikizo la damu. Inapendekezwa kutumia gramu zisizozidi 5 kwa siku.
Matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi. Watu wanaokunywa soda angalau 2 kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kuwa na protini kwenye mkojo wao. Protini kwenye mkojo ni moja ya dalili kuwa figo zako hazifanyi kazi kama zinavyotakiwa.
Kutopata usingizi wa kutosha. Usingizi wa usiku hauna faida kwako tu bali pia kwenye figo zako. Tishu za figo zinafanywa kuwa mpya tena wakati wa usiku hivyo kutolala usiku kunaweza kusababisha uharibifu wa figo zako.
Matumizi yaliyokithiri ya protini ya wanyama kama nyama nyekundu. Matumizi ya protini ya wanyama mara kwa mara kama nyama ya ng'ombe au nguruwe huongeza mzigo katika ufanyaji kazi wa figo