Mwanamke mwenye umri wa miaka 31, mkazi wa kata ya Cheyo, manispaa ya Tabora anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uangalizi wa matibabu baada ya kujaribu kuijua kwa kujichoma kisu tumboni kufuatia mgogoro wa kimapenzi.
Tukio hilo lilitokea Aprili 7, 2026 majira ya saa 9 mchana katika eneo la Cheyo ambapo mwanamke huyo ambaye jina halijatolewa alijichoma kisu tumboni na kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliotokea kati yake Mwanamke na mpenzi wake ambaye ni mwanaume wa miaka 33 anayejighulisha na biashara ya bodaboda katika eneo hilo.
Polisi wamesema uchunguzi unaendelea huku wakitoa wito kwa wananchi kutafuta msaada wa ushauri wa kutatua migogoro kwa njia sahihi ili kuepusha matukio kama haya.