Tabora: Aliyeua mtoto baada ya kumkuta mama yake na ARV ahukumiwa kifo

Tabora: Aliyeua mtoto baada ya kumkuta mama yake na ARV ahukumiwa kifo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Hukumu imetolewa na Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora dhidi ya Haruna Ndayanze baada ya kumkuta na hatia ya mauaji hayo kwa madai alibaini Mama wa mtoto anatumia Vidonge vya Kufubaza Virusi vya UKIMWI.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya, Demetrio Nyakunga alisema Mahakama imeridhika na ushaidi na hivyo mshtakiwa anahukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Upande wa Mashitaka uliowakilishwa na Mawakili, Merito Ukongoji na Sabrina Silayo ulidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 25, 2020 katika Kijiji cha Pozamoyo wilayani Kaliua.

==================

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, imetoa hukumu ya kunyongwa hadi kufa Haruna Ndayanze baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wa mkewe kwa madai kuwa alimkuta mama yake akimeza vidonge vya kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVS).

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Tabora, Demetrio Nyakunga alitoa hukumu hiyo baada ya kukasimiwa mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mahakama kuu.

Nyakunga alisema mahakama hiyo imeridhika na ushaidi uliotolewa mahakamani hapo na hivyo mshitakiwa Ndayanze ametiwa hatiani kwa kumuua Kusaga Magulu ambaye ni mtoto wa mkewe aliyezaa na mwanaume mwingine.

Upande wa mashitaka ukiwakilishwa na mawakili, Merito Ukongoji na Sabrina Silayo ulidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Januari 25 mwaka 2020 katika Kijiji cha Pozamoyo wilayani Kaliua.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo mshitakiwa ilimuua mtoto huyo kwa kumkata kwa panga shingoni, mikononi na sehemu nyingine za mwili.

Upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi 12 na ukadai mahakamani kuwa sababu za mauaji hayo ni mshitakiwa kumkuta mkewe, Stephania Alphoncy akimeza ARVs.

Hakimu Nyakunga pia aliwahukumu kunyongwa hadi kufa, Ally Shaban Kinyogoli na Ally Mtoni Kambongo baada ya kuwakuta na hatia ya kumuua Ally Rajabu, mkazi wa Kijiji cha Igalula wilayani Uyui.

HABARI LEO
 
Serikali iwanyonge au iwafunge maisha
 
Huyo alitakiwa akifika jela wampige mande masela wamalize ugwadu.Haiwezekani kukatisha maisha ya watu harafu unaenda kula msosi wetu sisi walipa kodi ...huyo unakabizi jamaa zinamla mande wiki mpaka anakufa ***** zake
 
Ndayanze,jina kama la kirundi

Ova
Kaliua na Ulyankulu Tabora imejaa wakazi wa jamii hiyo uliyoitaja.

Kambi ya wakimbizi ya Ulyankulu ilivyunjwa na wakazi wake kurudishwa kwao Burundi ama kupewa uraia wa Tz.
 
Back
Top Bottom