Tabora: Diwani na mkewe wafariki kwa ajali

Tabora: Diwani na mkewe wafariki kwa ajali

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1666677486983.png

Diwani wa Kata ya Kalola Wilayani Uyui (Tabora ), Sauji Daud na mkewe, Magdalena Richard wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo Jumanne Oktoba 25, 2022.

Akizungumza na Mwananchi leo, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Said Ntahondi amesema, diwani huyo na mkewe walikuwa katika gari yao binafsi wakitoka Kalola kuja Tabora mjini na ndipo gari lao lilipogongana na gari lingine uso kwa uso na wao kufariki papo hapo.

Amesema miili yao imepelekwa kuhifadhiwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete kwa ajili ya uchunguzi na taratibu zingine.

"Tunasubiri uchunguzi na taarifa nyingine za wana ndugu kabla ya kupanga mazishi yao," amesema.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom